.

Jumanne, 24 Septemba 2013

China yaruhusu upatikanaji wa mitandao ya Twitter na Facebook kwenye baadhi ya maeneo ya nchi ya hiyo.



China inajulikana kwa ku-block upatikanaji wa mitandao mikubwa duniani kama Facebook na Twitter kwenye nchi yao. Katika hatua hii mpya, nchi ya China imeruhusu upatikanaji wa mitandao hii kwenye “Free trade zone of Shanghai”.China Internet Network Information Center (CNNIC) wanasema nchi yao hivi sasa ina watumiaji wa internet zaidi 591 million, pia lengo lao kubwa la kuruhusu mitandao hii kupatikana kwenye maeneo haya ni kwa ajili ya wafanyabiashara wanaotoka nchi za nje kuingia China wasione tofauti na wanapokuwa kwao. “Lengo kuu ni kuwafanya wafanya biashara wote wajiskie wako nyumbani na wafanye biashara zao vizuri”, alisema mmoja wa maafisa wa China.

Facebook na Twitter zilifungiwa kupatikana ndani ya China tangu mwaka 2009 kutokana machafuko ambayo serikali ililaumu sana mitandao ya kijamii kuchangia.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni