Anti ASU (AMOS) Akiwa ndani ya kumbi za Starehe enzi zake.
Kama ni mpenzi wa taarabu na unatembea sana usiku katika kumbi mbalimbali hapa Dar es Salaam basi ni lazima utakuwa unamjua au unamfahamu shoga maarufu hapa jijini aitwae "Aunt Asu" mtoto wa magomeni mapipa.
Mtaalamu huyu wa kuwabandika kope akina dada ameuambia mtandao wa taarabuzetu kwamba ameacha kazi ya ushogaa na kwa sasa ameokoka na amesha badili jina anaitwa "AMOS".
Anti Asu ambaye pia ameamua kuokoka na kukiri hadharani kwamba hataurejea kamwe ushoga, inaelezwa kwamba kwa sasa anatafuta mke wa kumzalia watoto na ambaye atampa mapenzi ya dhati.
Imedaiwa kwamba, hivi karibuni Othuman alijisalimisha katika kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), lililopo Magomeni Mikumi jijini Dar es Salaam ambako alitubu dhambi zake.
Mwandishi waetu aliamua kuingia mzigoni kufuatilia `ishu’ hiyo ambapo alifanikiwa kumnasa Othuman akiwa katika saluni moja ya kike iitwayo Emmy’s iliyopo Magomeni Mapipa jijini anakofanya kazi.
Alipoulizwa kuhusiana na taarifa za kuukana ushoga, kijana huyo alithibitisha ni kweli ameacha tabia hizo na kwa sasa ameokoka baada ya kubadili dini kutoka kwenye Uislamu na kwenda kwenye Ukristo akiitwa Amos.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni