Jinsi ya kuchagua jinsia ya mtoto "Nina
kukubali uwezo wako kiushauri na kiuzoefu,Umejaliwa!!..Mimi ni kijana
wa kiume mwenye umri wa miaka 27,nina mchumba wangu na tuko kwenye
harakati za kufunga ndoa.
Tatizo langu ni hili: Napenda sana
first born wangu awe wa kike;[tei tei.....],na ninasikia kuna namna
fulani ya kuweza kupanga jinsia ya mtoto japo ni kwa majaliwa ya mungu.
NIFANYEJE???? Naomba unisaidie jamanii!! Wako B.Z"
*****************************
Dinah
anasema: Ahsante, Nashukuru sana. Ni kweli kuna namna ya kuchagua
Jinsia ya mtoto kabla Mimba haijatungwa lakini bado haijathibitishwa
Kisayansi/Kitaalam.
Kupata mtoto wa Kike sio ngumu sana kama
ilivyo kwa mtoto wa kiume + inategemea zaidi kwenye uwingi wa jinsia
hiyo upande wako(familia ya mwanaume).
Mbegu zinazosababisha
mtoto wa kike "hutembea" taratibu kuelekea kwenye Yai na huishi kwa
masaa 72-Wiki....hivyo wewe na mkeo hamtahitaji kusubiri "tarehe"
maalum.
Kama kwenu au kwa baba mdogo/ mkubwa kuna wanawake wengi basi unaweza ukafanikiwa kupata Binti bila taabu kabisa.
Ila epuka kufanya mapenzi tarehe ambazo mkeo ajae anakaribia kupevusha Yai....fanya mapenzi baada ya hedhi na wiki mbili baadae.
Mbegu
zinazosababisha mtoto wa kiume zipo "faster" na hufa haraka, hivyo kama
unataka mtoto wa kiume inabidi kutegea "tarehe" maalum ili Mbegu
iliwahi yai likiwa njiani...
Japokuwa suala la mtoto wa kiume
linategemea zaidi upande wa Mwanamke, ikiwa kwako kuna wanaume wengi au
idadi sawa na wanawake, urahisi wa kupata mtoto wa kiume ni kubwa.
Sehemu
ya maelezo yangu ni kutokana na uzoefu wangu binafsi, tulipotaka mtoto
wa kwanza awe wa Kiume tulikuwa tunafanya kwa kufuata "tarehe" maalum +
mikao maalum(hakuna kifo cha mende wala vijiko)!!
Mtoto wetu wa Pili amble ni wa kike, hatukufuata "tarehe" maalum...
Kifamilia, idadi ya wanaume kwetu ni kubwa kuliko wanawake.
Wengine wataongezea... Mapendo tele kwako..
Credits: Dinahicious Blog |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni