Staa huyo aliyeanza ‘kuhiti’ tangu akiwa na umri mdogo, alinaswa na kamera zetu usiku wa Jumatano iliyopita ndani ya Club Bilicanas, Dar es Salaam.
Ilikuwa saa 6:39, paparazi wa Risasi Jumamosi alimtia machoni Aunty Lulu kwa mara ya kwanza ndani ya klabu hiyo, kulikokuwa na shoo ya Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’.
Baada ya kuzunguka kwa dakika mbili hivi, Aunty Lulu alitenga makalio jirani na moja ya kaunta za klabu hiyo na kuanza kukata monde a.k.a maji ya mende ambayo yalimchakaza na kumuacha hoi.
Kama ilivyo kwa msemo, ‘ulevi noma, funda moja tu la ziada linaweza kukuumbua’ ndivyo mambo yalivyomtokea puani Aunty Lulu, kwani mwisho alikuwa taabani na kufanya yasiyo na heshima.
Jioni ya siku ya tukio, Aunty Lulu katika mawasiliano na mmoja wa mapaparazi wetu, aliandika SMS: “Jamani sasa hivi nipo ‘bize’ na masomo. Nipo kwenye mitihani ndiyo maana sipatikani.”
POMBE ZILIPOISHA (ALHAMISI ASUBUHI)
Baada ya kupigiwa simu na paparazi wetu kumjulia hali kutokana na jana yake kuwa tilalila alijibu: “Jamani mimi sikumbuki kitu, rafiki zangu ndiyo wameniambia asubuhi hii. Nadhani pombe sasa zinanishinda, hii ni hatari.”
CHUO CHA AUNTY LULU
Hivi sasa, Aunty Lulu anasomea cheti cha uandishi wa habari kwenye Chuo cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC) jijini Dar.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni