.

Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo UDAKU. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo UDAKU. Onyesha machapisho yote

Jumatatu, 10 Novemba 2014

Alichoandika Hemedy PHD kuhusu msanii wa Tanzania aliesema hafanyi tena collabo na Wabongo.

Screen Shot 2014-11-10 at 11.03.32 AMMwigizaji/Mwimbaji Hemedy PHD ni miongoni mwa mastaa wa Tanzania ambao hutumia sehemu ya muda wao pia kuandika kwenye mitandao ya kijamii yake ya moyoni ama kuwafikishia taarifa mashabiki wake.
November 10 2014 Hemedy aliandika tweet ikisema >>> ‘Mtu anasema hategemei kufanya collabo na msanii wa bongo ikiwa ngoma zake zote kabebwa na collabo, fikiri kabla ya kuzungumza‘
Hemedy ameandika tweet hii siku kadhaa baada ya msanii Shetta kusema kwa sasa hafikirii kufanya collabo na Wasanii wa Tanzania bali anafanya mpango wa kujipenyeza kimataifa zaidi akisema ‘nimefanya collabo nyingi na Wasanii wa Tanzania ndio maana siko tayari kufanya tena hivyo nikawa nawaza mawili, nifanye collabo na msanii wa kimataifa au kutoa wimbo peke yangu?‘
Kwenye tweet nyingine Hemedy aliiandika kumuhusu President Jakaya ambae yuko Marekani alikokwenda kutibiwa.
 Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa

Jumapili, 26 Oktoba 2014

SIRI IMEFICHUKA: MTIFUANO KATI YA DIAMOND NA ALIKIBA KUMBE CHANZO NDIO HIKI HAPA.

Kama umefuatilia katika wiki hii kumekuwa na vuguvugu kali linaloendelea kati ya Mahasimu hawa wawili, sasa wengi wakiwa hawajui nini chanzo cha Bifu kubwa linaloendelea kati ya Diamond Platnumz na Ali Kiba.



Katika hali ya kutaka kujua ukweli mtangazaji wa kipindi cha XXL alimtandika
swali la kizushi Ali Kiba kuhusu Bifu hilo linaloendelea mpaka sasa huku akitaka kujua chanzo kikubwa cha yeye na Diamond na yeye kuhitiliafiana. Ali aligoma kabisa kuelezea chanzo cha 

Jumatano, 22 Oktoba 2014

JE UNAMJUA MKE WA MSANII JB BONGE LA BWANA? BASI MCHEKI HAPA

.



Katika pita pita mtandaoni tumekutana na picha hizi za JB a.k.a Bonge la bwana akiwa ameziweka katika akaunti yake ya Instagram na kuonyesha ni jinsi gani anajivunia kuoa na kuwa na

mke mzuri kama huyu. Tazama picha hapo chini uone ni jinsi gani jamaa anajiamini na anampenda mke wake na haoni shida kumuweka mtandaoni ili mashabiki zake wamfahamu shemeji na wifi yao.

LOL! ROSE NDAUKA AITIA AIBU BONGO MUVI...ANASWA AKINYEMELEA PENZI LA T.I

MAHABAT! Katika hali ya kushangaza, staa wa sinema za Kibongo, Rose Ndauka alinaswa akihaha kumtia kwenye himaya ya penzi lake Rapa kutoka Marekani, Clifford Joseph Harris ‘T.I’.




Rapa kutoka Marekani, Clifford Joseph Harris ‘T.I’.
Tukio hilo lililofuatiliwa hatua kwa hatua na mwanahabari wetu lilitokea usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita katika Viwanja vya Leaders Club wakati Mmarekani huyo alipokuwa akitumbuiza kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2014.
Awali, Rose ambaye aliongozana na Mtangazaji wa Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’, mwigizaji Jacqueline Pentezel ‘Jack wa Chuz’ na mumewe, Gardner Dibibi, alisikika akiwaambia wenzake hao kuwa piga ua ataondoka na msanii huyo anayetamba na wimbo wa No Mediocre.
“Kama hamuamini mtaona, kifupi T.I ni shemeji yenu na hilo nitawaonyesha hapahapa pindi nitakapokaa naye,” alisikika Rose.
Kutokana na kuwalazimisha kwa muda mrefu wenzake hao wakubali wakiwa viwanjani hapo, ilifika wakati kila mmoja alikubaliana na hoja yake na kumuita ‘bebi’ wa T.I.
“Haya bwana, shem (T.I) anapanda saa ngapi?,” alisikika Gardner.
Staa wa sinema za Kibongo, Rose Ndauka.
Kama hiyo haitoshi, kuna wakati, Rose ambaye alionekana kama ulabu upo mahali pake, alitoweka katika kundi la wenzake kwa takriban dakika 20 akidai anakwenda nyuma ya jukwaa kumfuata T.I.
Hata hivyo baada ya muda alirejea na kudai imeshindikana kumuona kwa muda huo lakini atajitahidi hadi shoo itakapokwisha, atakuwa ameshakaa naye na kuzungumza naye kwa kirefu.
“Sijamuona ila hamna shida, nitamuona tu kabla shoo haijaisha,” alisikika Rose ambaye juzikati alimwagana na aliyekuwa mchumba’ke wa muda mrefu, Malick Bandawe.
Hadi mwanahabari wetu anaondoka viwanjani hapo, mrembo huyo mwenye mvuto wa aina yake hakuwa amefanikiwa kumtia mikononi rapa huyo.

Ijumaa, 10 Oktoba 2014

NI KWELI OMMY DIMPOZ!!!



-2
Kwa muonekano wa Ommy Dimpoz umeashilia kweli Kigoma ndio nyumbani “Home Sweet Home” kutokana na mandhari ya treni na kama unavyojua usafiri mkubwa kwa miaka hiyo ulikuwa ni gari moshi aka treni, sasa hapa Ommy ndiyo anaingia Dar au? ila katisha sana.
All in all usikose kuzidi kuangalia kichupa cha ‘Ndagushima’ kinachofanya poa kwenye luninga.

Jumamosi, 4 Oktoba 2014

MKONGO MAN BAADA YA KUMCHEZEA WOLPER SASA ADAI ANAMTAKA LULU KWA GHARAMA YOYOTE ILE

Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwami inayosaidia watu wasiojiweza na yatima, inayofanya kazi nchi za Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mwami Rajabu ‘Mkongo’ ameibuka na madai mazito kwamba baada ya ‘kumalizana’ na mastaa wa Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe na Husna Maulid, kwa sasa anamtaka mwigizaji Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ kwa gharama yoyote.

Mwami Rajabu ‘Mkongo’.
Akizoza na gazeti hili ndani ya Hoteli ya Double Tree iliyopo Masaki, Dar, mapema wiki hii, Mwami ambaye ni raia wa nchi ya Kongo alifunguka kwamba, amewahi kudaiwa kutoka na wasichana kibao Bongo lakini yeye ni mume wa mtu anayejiheshimu na hao wanawake aliotajiwa kutoka nao aliwahi kuwa nao karibu kwa lengo la kutaka kufanya nao kazi tu na si vinginevyo.
“Unajua watu wamenitajia eti nimetoka na Wolper, Husna mara Wema, si kweli, hawa watu mimi niliwahi kukutana nao Nairobi (Kenya) kwa lengo la kufanya nao biashara lakini mwanamke ambaye ananilaza macho na hata nikimpata siwezi kuficha penzi ni Lulu,” alisema Mwami bila soni.
Mwigizaji Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’.
Jamaa huyo ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 35 na kuendelea huku akiwa na mke na watoto sita alisema kwamba, akipatikana mtu wa kumuunganisha na Lulu kwa gharama yoyote atafurahi kwani ni mwanamke wa ndoto zake.
“Wote siwataki lakini nikimpata Lulu simwachi nampenda sana tena sana,” alisema jamaa huyo kwa nyodo akionekana ni mtu ambaye fedha zimemtembelea.
Jitihada za kumpata Lulu ili kusikia analichukuliaje suala hilo hazikuzaa matunda kwani simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa na hata alipofuatwa nyumbani kwake Mbezi Beach, Dar, hakuwepo hivyo juhudi za kumpata zinaendelea

Alhamisi, 2 Oktoba 2014

YALAAAAAAH! USALITI MAPENZINI: USIKURUPUKE, FAHAMU HATUA KUMI ZA KUCHUKUA BAADA YA KUSALITIWA!



Katika maisha ya kimapenzi hakuna kitu kinachouma kama kusalitiwa, tena kusalitiwa kunakouma zaidi ni pale unapobaini mpenzi wako kampa penzi mtu unayemjua halafu ukijilinganisha wewe na huyo aliyepewa unashindwa kuelewa kilichomshawishi mpenzi wako.
Lakini licha ya kwamba usaliti si kitu kizuri, watu wamekuwa wakisalitiana, tena sana tu. Inafika wakati unashindwa kuamini kama yupo mtu ambaye hajawahi kumsaliti mpenzi wake.
Niseme tu kwamba wapo wachache waliotulia ila asilimia kubwa ya walio kwenye uhusiano ni wasaliti hata tafiti zimethibitisha hilo.


Kama hali yenyewe iko hivyo, cha kujiuliza ni kwamba unapobaini mpenzi wako kakusaliti ni kipi unachotakiwa kufanya?
Je, ni kuamua kunywa sumu kama ambavyo wamekuwa wakifanya wengine? Sidhani kama huo ni uamuzi sahihi.


Mtaalam wa masuala ya mapenzi James Johnson kutoka Marekani amependekeza mambo 10 unayoweza kufanya baada ya kubaini kuwa mpenzi wako amekusaliti.

1. Kubaliana na kilichotokea
Kama kishakusaliti ni tukio ambao limeshatokea na haliwezi kufutika. Kubali kuwa umetendwa, huzunika lakini mwisho liache lipite ili uweze kujipanga upya.

2. Usijilaumu
Wapo ambao wakishasalitiwa hujuta kukubali kuingia kwenye uhusiano na watu waliowatenda. Utamsikia mtu akisema ‘najuta kumkubalia awe mpenzi wangu’. Kujilaumu kwa namna hiyo hukutakiwi kwani kutakufanya uzidi kunyong’onyea.

3. Jitoe
Jifanye kama vile aliyesalitiwa siyo wewe bali ni rafiki yako kisha jiulize ungemshaurije? Ushauri ambao ungempata basi uchukue kisha uufanyie kazi.

4. Pima ulivyoathirika
Je, kitendo cha mpenzi wako kukusaliti kimekukosesha imani juu yake? Kama ni hivyo, unadhani una sababu ya kuendelea kuwa naye au unahisi madhara aliyokupatia huwezi kumvumilia?

5. Mpasulie ukweli
Kwa vyovyote utakavyoamua ni lazima umweleze juu namna alivyokuumiza kwa usaliti wake. Hata kama utampa nafasi nyingine lazima ajue jinsi alivyokuumiza ili iwe changamoto kwake.

6. Chunguza kwa nini kakusaliti
Usiliache likapita hivi hivi, unatakiwa kujua sababu ya yeye kukusaliti. Je, kuna ambacho anakikosa kwako au ni tamaa zake tu? Jibu utakalolipata litakusaidia katika maisha yako ya kimapenzi.

7. Usikubali akulainishe
Huenda huyo mpenzi wako ni ‘msanii’ na anaweza kukulainisha kwa maneno ambayo yanaweza kukufanya ukalichukulia tukio hilo kiurahisi. Kuwa na msimamo na eleza hisia zako kwa uwazi.

8. Amua kusuka au kunyoa
Likishatokea hilo jaribu kuzungumza na moyo wako. Uamuzi wa kuendelea kuwa naye au kumuacha uuchukue bila shinikizo. Hata kama kakuumiza, kama unadhani unaweza kumpa nafasi nyingine mpe ili usije ukajuta baadaye kwa kumkosa lakini kama unaona moyo wako unamkataa, muache.

9. Msamehe
Kwa uamuzi wowote utakaochukua ni lazima uwe tayari kumsamehe ili kuliondoa dukuduku lako rohoni. Kutokumsamehe kunaweza kukufanya ukawa unaumia kila wakati na kukosa amani.

10. Iwe fundisho kwako
Chukulia tukio hilo kama fundisho kwako. Huenda wewe ndiye uliyechangia kusalitiwa, kama ni hivyo badilika ili yasije yakakukuta kama hayo utakapokuwa na mwingine. Pia kama kusalitiwa kumetokana na kutoridhika kwa mpenzi wako, kuwa makini wakati wa kuchagua mwingine wa kuwa naye.

AIBU KUBWA: MKE, MUME WAVUANA NGUO LIVE WAKIZICHAPA HADHARANI..WAFUNGA MTAA KWA SINEMA YA BURE!


Hii ni aibu kubwa! Njemba mmoja aliyefahamika kwa jina la Zeno na mkewe Mwajuma Mtata, wakazi wa mtaa Mrefu, Kigogo-Luhanga jijini Dar wamenaswa wakiangusha bonge la timbwili barabarani na kusababisha umati wa watu kujikusanya eneo hilo kujionea ‘sinema’ ya bure.Timbwili zito likianza kati ya njemba mmoja anayefahamika kwa jina la Zeno na mkewe Mwajuma Mtata. Tukio hilo lililofananishwa na muvi ya kivita lilitokea usiku wa Jumanne iliyopita ambapo chanzo kimedaiwa kuwa ni mwanamke huyo kutelekeza jikoni kitoweo cha maini ya mbuzi na kwenda baa kupata kilaji. 
Kwa mujibu wa chanzo makini, siku ya tukio, Zeno alirudi nyumbani mida ya jioni mkononi akiwa na kifurushi chenye maini ya mbuzi pamoja na mazagazaga mengine zikiwemo ndimu, tangawizi, pilipili hoho, nyanya na vitunguu kupokelewa na ‘mai waifu’ wake huyo.

AIBU: MKE WA KIONGOZI AKIMBIA MTAA BAADA YA PICHA ZAKE ZA UC*H*I ZIMEBANDIKWA KWENYE ZA UMEME


 
Aibu ya mwaka imemkuta huyu mama baada ya picha zake kubandikwa kwenye guzo za umeme,wamefanya hivi kutoka kana na tabia mbaya ya huyu mama kugawa uroda kwa vijana wadogo

Jumanne, 30 Septemba 2014

MCHUNGAJI ALIYEWALISHA WAUMINI MAJANI AJA NA MPYA..SASA AWAPONYA WAGONJWA KWA KUWAKANYAGA KANYAGA

Yule Pastor Mwenye Vituko Vingi Kutoka South Afrika anayejulikana kwa jina la Lesego Daniel amekuja na Mpya baada ya kuwalisha majani waumini na kubadilisha petrol kuwa Juice ya Apple , Sasa eti anawaponya Waumini wake ambao wanasumbuliwa na magonjwa kwa kuwakanyaga migongoni...Angali Picha Hapo Juu

DUH! SOMA ALICHOKIANDIKA 'MASANJA MKANDAMIZAJI' BAADA YA DIAMOND KUMZAWADIA GARI 'WEMA'


Alhamisi, 25 Septemba 2014

What a new woman for a King of Rhymes Afande Sele…


Na Musa Mateja
MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya Seleman Msindi ‘Afande Sele’, juzikati alinaswa akiwa na demu mpya akiwa ni siku moja tu baada ya kufanyika kwa 40 ya aliyekuwa mzazi mwenzake, marehemu mama Tunda.

Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Seleman Msindi ‘Afande Sele’,akiwa na mpenzi mpya.
Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Septemba 21 mwaka huu ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati staa huyo aliyekuwa mmoja wa watoa burudani katika tamasha la Fiesta, alipoonekana akiingia akiwa ameambatana na mrembo mmoja akiwa ameshikana naye kimahaba.
Akiwa ndani ya uwanja huo, mkali huyo wa mashairi yenye vina kwa muda mwingi alikuwa pamoja na msichana huyo ambaye hakufahamika jina, wakiwa na dalili zote za wapendanao.

Mkali wa ‘Rhymes’ Bongo, Seleman Msindi ‘Afande Sele.
Alipoulizwa juu ya suala hilo, Afande Sele alicheka na kumtaka paparazzi wetu kuachana na masuala hayo aliyoyaita binafsi, badala yake asubiri apande jukwaani apate picha za kazi atakayofanya

Jumapili, 21 Septemba 2014

Wema Akataa kumzalia Diamond Kuogopa Kupoteza Mvuto Na Umaarufu….Diamond Amrushia Dongo


Diamond Platnumz kwa muda sasa amekuwa akimwambia mpenzi wake Wema Sepetu abebe mimba kwasababu yeye anataka mtoto lakini Wema amekuwa mgumu kukubali kudungwa mimba na Diamond kwasasa kwa madai kuwa hayupo tayari kuzaa muda huu sababu ikiwa ni kuwa atapoteza mvuto wake kiumbo na pia kuchuja kiumaarufu, kitu ambacho hakitaki.
 
“Ni muda sasa Diamond anataka mtoto tatizo Wema hataki, anaogopa kushuka umaarufu na pia kupoteza umbo lake lenye mvuto.
 
“Kitendo hicho kimemuweka njia panda Diamond kwa sababu pesa anayo ya kutosha kulea mtoto ila haelewi kwanini Wema hataki wapate mtoto  eti  kwa kisingizio cha kupoteza fame yake na umbo” 
 
Hata hivyo Diamond juzi kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii aliweka post inayoshabihiana na maelezo ya chanzo hicho. Diamond ni kama alikuwa amerusha Dongo hilo kwa Wema kwa kuandika …
WEMANADIAMONDi
 
“Kwa mtazamo wangu mimi naona kuzaa hakumfanyi mtu azeeke au awe wa kizamani, ni tabia tu ya mtu mwenyewe…. na ndio maana dada zetu kama Beyonce, Nancy sumary, Kim Kardashian na kadhalika wana watoto na still wanafanya vizuri…..Au we mtazamo wako ukoje?…….. “
 
Vile vile mapema wiki hii gazeti moja la burudani liliandaka habari inayokaribiana maana na hii kuwa Wema hataki kuzaa kuogopa kupoteza mvuto wake na umaarufu

Jumamosi, 20 Septemba 2014

KAMA ULIKUWA HUJUI NI KWAMBA ALI KIBA ANA WATOTO WATATU NA HAWA NDIO MADEMU ALIOZAA NAO AKIWEMO .....


Mwanamuziki maarufu wa Bongo Fleva nchini Ali Kiba amesema kuwa ana watoto watatu na kila mmoja ana mama yake.
 
Akizungumza na paparazi kiba aliyetoa nyimbo mbili mpya hivi karibuni alisema kuwa kati ya watoto hao mmoja anaishi nae, wa pili yupo  Dar es salaam na mama yake na watatu anaishi Uingereza na mama yake.

Ijumaa, 12 Septemba 2014

ETI WEMA, DIAMOND NA AUNT WANATAJWA KWENYE LIST YA MICHEPUKO HATARI SANA!

Ni tamaa ya ngono au ni nini? Hivyo ndivyo unavyoweza kujiuliza baada ya kubainika kwamba mastaa watatu Bongo, Wema Isaac Sepetu, mpenzi wake Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Aunt Ezekiel Grayson wanatajwa kwenye mchepuko hatari wa kuzungukana kimalovee, Ijumaa lina kila sababu ya kukujuza.
Mastaa watatu Bongo, Wema Isaac Sepetu, mpenzi wake Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Aunt Ezekiel wakiwa katika picha ya pamoja.
KILA KUKICHA
Ishu hiyo imebumburuka baada ya hivi karibuni mastaa kutengeneza vichwa vya habari kila kukicha kuhusiana na mambo yao hayo.
AUNT NA MOZE IYOBO
Duru za kihabari zinaonesha kwamba hivi karibuni mwigizaji Aunt, bila ya kupepesa macho huku akijua dhahiri kuwa ni mke wa mtu, Sunday Demonte alifungua kinywa na kuapa kuwa hawezi kuachana na mume wa mtu, Moses Peter Iyobo ‘Moze Iyobo’ ambaye ni densa wa Diamond.
Aunt alitamka maneno hayo akijua fika kuwa Moze Iyobo ni mume wa mwanamke aitwaye Mwengy ambapo wanaishi Mbagala jijini Dar, wakiwa wamejaliwa mtoto mmoja.
Mume wa mtu, Moses Peter Iyobo ‘Moze Iyobo’ akiwa na ‘Diamond Platnumz’.
AUNT KIOO CHA JAMII?
“Dah! Natambua kuwa msanii ni kioo cha jamii lakini si kwa Aunt, hana hadhi ya kuitwa kioo cha jamii kutokana na tabia yake ya kuchepuka wakati ni mwanandoa,” alidai mmoja wa watu wake wa karibu.
Mdau mwingine wa sanaa za nyumbani aliyejitambulisha kwa jina la Said, mkazi wa Mwananyamala jijini Dar, alimshangaa Aunt kukiri hadharani kuwa ana uhusiano usiofaa na Moze Iyobo ambaye ni shemeji wa Wema kwa Diamond na yeye (Aunt) ni shosti wa Wema.
Alisema kwamba, kwa hadhi yake, Aunt hakupaswa kutoa kauli hiyo ili watu waendelee na minong’ono kuhusiana na yeye (Aunt) tofauti na alivyofunguka bila aibu ukizingatia ni mke wa mtu.
“Unajua kwa nini nasema Aunt anajidhalilisha au anawadhalilisha wanawake wenzake ni pale anapokiri kuwa ndoa yake ipo tena bado anampenda mumewe huku anakuja kusema kuwa anampenda Moze Iyobo, huo kama siyo mchepuko ni nini?” alihoji Said.
‘Moze Iyobo’ akiwa na familia yake.
WEMA NA DIAMOND
Uchunguzi ulionesha kwamba, huku wakijua kila kitu waliwaruhusu Ahmed Hashim ‘Petit Man’ (Toto ya Wema) na Esma Platnumz ‘kuchepuka’ huku Petit akiwa ni shemeji wa Diamond kwa Wema.
Pia Diamond alifanya ‘misteki’ kumuacha mdogo wake, Esma ‘kuruka’ na Petit kwa kuwa ni shemeji yake.
KAJALA ANAINGIAJE?
Ilibainika pia kwamba Petit aliwahi kuchepuka na mwigizaji Kajala Masanja ‘Kay’ ambaye ni mke wa mtu, Faraji Agostino aliyeko gerezani na hilo likiwa wazi hata kwa hao akina Wema na Diamond.
“Hebu jaribu kuangalia huo mzunguko na mkanganyiko uliopo hapo. Yaani ni aibu tosha,” alisema mdau mwingine kuhusiana na ishu hiyo.
'Petit Man' akipozi kimahaba na Kajala Masanja, 'K'.
STEVE NYERERE AANIKA AIBU YAO
Hivi karibuni kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar, Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ aliwavaa mastaa hao na kuanika aibu yao huku akimshutumu Aunt ambaye alifika maeneo hayo akiwa ameongozana na mpenzi wake huyo wa sasa, Moze Iyobo.
Steve alisikika akimwambia Aunt kuwa hamtendei haki Moze Iyobo na anamnyima uhuru mkubwa kutokana na umri wake ambao anaweza hata kumzaa.
“Unajua wewe Aunt unastahili kuwa na mtoto mkubwa mwenye umri usiokuwa tofauti na huyu Moze Iyobo.“Hivi kwa nini unajidhalilisha kiasi hicho kwani wazee wenzako hujawaona hadi kumbemenda mtoto wa watu?” alisika Steve akimpasha Aunt kwa sauti ya juu.
'Petit Man' yule yule akiwa na dada yake 'Diamond Platinum', Esma.
NI SHARTI LA DIAMOND KWA WEMA
Akiendelea kumpasha Aunt, jamaa huyo alikwenda mbali zaidi pale alipomwambia Aunt kwamba anahisi kuwa uhusiano wake na Moze Iyobo ni sharti kutoka kwa Diamond kumpa Wema ili alifanyie kazi na kumwambia kuwa ahakikishe yeye (Aunt) anakuwa na Moze na Petit Man amuoe Esma.
“Unajua hivi karibuni baada ya Diamond kuandika yale maneno katika Mtandao  wa Instagram, nilisikia waliachana sasa naona Diamond alimwambia Wema kama unataka nikurudie ahakikishe kuwa wewe Aunt unakuwa na huyu mtoto (Moze Iyobo) halafu yule dogo mwenye rasta sijui mnamuita Petit Man ahakikishe anamuoa Esma dada yake Diamond,” alisema Steve.
Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ akifafanua jambo.
AUNT AWA MBOGO
Baada ya Steve kutoa dukuduku lake mwigizaji huyo aligeuka mbogo na kumwambia Steve kuwa amuache kwa raha zake kwani anampenda Moze Iyobo hata aseme nini hawezi kumuacha.
“Hata uongee nini Steve, siwezi kumuacha mpenzi wangu, nampenda sana na hayo masharti unayoyasema kuwa ameyatoa Diamond unayajua wewe, niachie nile raha zangu na Moze wangu,” alisema Aunt akimwangushia Moze Iyobo bonge la ‘kisi’.
KUTOKA IJUMAA

Ni kweli wasanii ni kioo cha jamii lakini kwa kuwa wamekuwa ‘vichwa ngumu’ kutenda yale yanayowafanya kuwa vioo vya jamii ni vema jamii yenyewe ikachuja mema na kuyachukua kisha kuwaacha wabaki na hayo machafu yao.

Alhamisi, 11 Septemba 2014

LAANA: BAADA YA KUACHANA KIJANA AVUJISHA PICHA ZA DEMU WAKE AKIMNYONYA NANILIUU AIBU 18+


VIDEO YA MTOTO WA WAZIRI AKIMLA URODA DEMU NDANI YA GARI!!!!

Video imezagaa mtandaoni ikimwonyesha mtu ambae inasadikiwa kuwa ni mtoto wa wawaziri wa mambo ya nje....Hannah Tetteh...Nouma sana

JIBABA LA BAMBWA LIKIMTATUA MALINDA BINTI WA MIAKA 15!!!!...#MuguUtusamehe

HAPA WALIKUWA KITANDANI.
Hii ni NOUMA...Mzee anakadiliwa kuwa na umri wa miaka isiopungua 56 amekutwa LIVE akin naniliuu na binti amabae inasemekana ni ndugu wa mkwe....mwenye umri wa miaka chini ya kumi na-SITA.....Baada ya Watu wa karibu kushtukia mchezo akiwemmo mkeo..wakapanga mtego wa kumnasa mzee huyu.... Hii imeripotiwa kutoka nchini Nigeria

PICHA ZA FARAGHA ZA PHD HEMEDI AKIWA CHUMBANI NA MCHEPUKO ZASAMBAA KWA KASI MTANDAONI, TAZAMA HAPA

Ikiwa kuna matetesi kibaokwamba jamaa anafunga ndoa phd hemedi kuna picha za mahaba zenye utata
zimevuja akiwa anaonekana yuko chumbani na demu ambaye bado hajafahamika kama ndio yule mke mtarajiwa au ni mchepuko


Diva Afunguka tena…Adai Zitto Kabwe ni mume wake na anatambulika kisheria



Mtangazajiwa Kipindi cha Ala za Roho kinachorushwa kupitia Radio Clouds FM ya jijini Dar, Loveness Malinzi ‘Diva’ kwa mara ya kwanza, amejilipua kuzungumzia uhusiano wake na Zitto Kabwe kwamba walikuwa mke na mume.
 
Katika mahojiano maalum na mwanahabari wetu jijini Dar juzi, Diva alisema anashangazwa na baadhi ya vyombo vya habari  kumnyima uhuru wa kuongelea suala lake na ‘zilipendwa’ wake huyo wakati kisheria yeye ni mke wake hivyo anapaswa kuzungumzia kutengana kwao.
 
“Ninyi mnayaongelea mambo ya Zitto na mimi juu kwa juu tu hamjui kama mimi nimeishi naye kama mke na mume nyumbani kwake Masaki (Dar), sasa nini kilisababisha penzi letu kuvunjika watu hawajui, nina ushahidi wa kutosha lakini wanaongeaongea tu,” alisema Diva.Akaongeza: 
 
“Sasa ninavyojua mimi kwa sheria za nchi, mwanamke na mwanaume wakiishi pamoja kwa zaidi ya miezi sita tayari ni mke na mume. Hawezi kuniacha kirahisirahisi tu.”
zitto
 
Diva alikwenda mbele zaidi kufuatia kauli ya Zitto aliyoitoa hivi karibuni kupitia Kipindi cha Mkasi kinachorushwa hewani na Runinga ya East African Television ‘EATV’ na mtangazaji Salama Jabir.
 
Zitto aliulizwa ana uhusiano gani na Diva, naye akajibu ni mtu wanayefahamiana tu lakini si mpenzi wake.
 
Ilidaiwa kwamba, majibu hayo ya Zitto kwa Salama ndiyo yaliyoibua hasira ya Diva hadi kufikia hatua ya kutupia kwenye ukurasa wake wa Instagram, e-mail aliyodai aliwahi kutumiwa na Zitto siku za nyuma akimtaka asiwe anaweka wazi uhusiano wao kwa sababu atachafuka kisiasa.
Diva
Diva
 
E-mail ilisomeka  hivi:
“Unanikosea sana ujue unapoweka mambo yetu hadharani. Ninaonekana siwezi kuwa kiongozi kwa sababu nashindwa ku-handle masuala yangu binafsi.
“Madhara uliyoyafanya ni makubwa sana. Wapinzani wangu wa kisiasa watayatumia sana dhidi yangu.
 
“Ungekuwa unajua madhara yake usingethubutu kufanya ulivyofanya mara tatu sasa. Sijui nia yako nini, ila ipo siku utajua umenikosea sanasana.”
 
Swali la mwandishi:
Je, Zitto akikubali kufuata huo utaratibu uwe mkewe utamuacha GK ambaye umekuwa ukimtangaza kuwa mpenzi wako?
Diva: Hilo nitakujibu baadaye.
 
Siku za karibuni, baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti uhusiano wa Diva na Zitto bila kuzama kwa undani.
 
Kufuatia Diva kutupia madai hayo mtandaoni na kudai yeye ana hadhi ya mke kwa Zitto na kauli ya Zitto kwenye runinga kwamba Diva si mpenzi wake, baadhi ya watu waliozungumza na Amani walionesha kwenda kinyume na mtangazaji huyo.
 
Wengi walidai kwamba wana kumbukumbu zilizonyooka kwamba Diva amewahi kujinadi kutoka na Mbongo Fleva, Gwamaka Kaihula ‘Crazy GK’.

“Sasa Diva anavyodai ni kama mke wa Zitto mbona anamtangaza mwanaume mwingine?” Alisema mkazi mmoja wa jiji aitwaye Yuda.
 
Naye Ismail Juma, mkazi wa Kigogo, Dar alisema aliwahi kusoma kwenye vyombo vya habari kwamba Diva anapumzika na mwanamuziki kutoka Kenya, Jackson Makini ‘Prezzo’ kiasi cha kumzalishia bifu na demu wa jamaa huyo, Huddah Monroe. “Diva awe na aibu basi, asikurupuke wakati yeye mwenyewe si msafi kivile,” alisema Ismail.
 
Kufuatia madai hayo, kwa muda wa siku saba, Amani limekuwa likimsaka Zitto kwa njia ya simu lakini bila mafanikio.Watu wa karibu naye walipoulizwa alipo, walisema wanachojua ana shughuli zake nchini Zambia.