.

Alhamisi, 25 Septemba 2014

KIGOGO WA ZAMANI CHADEMA ATOBOA SIRI ZA MAANDAMANO YAO YASIYOKWISHA KILA SIKU LIVE!!




   

Default CHADEMA huwalipa waandamaji

Ndugu,

Wakati maandamano yametangazwa nchi nzima na chama chetu, na kwa kweli mimi nilisema sitashiriki kwa sababu ambazo nilieleza, na zote zimeonekana kuwa kweli, dhamiri yangu imenituma kuongea jambo jingine ambalo laweza kusaidia baadhi ya watu. Ingawa najua chama changu hakitafurahishwa na hii revelation, lakini napenda nihukumiwe kwa kuutumikia ukweli.

Ndugu, wengi wa makamanda wetu hujitolea kufanya kazi za chama. Na kwa kweli umati wa wanaojitokeza kwenye shughuli za chama chetu CHADEMA kama mikutano ya hadhara ama maandamano, huja wenyewe bila kupewa fedha. lakini hii siyo kwa wote.

Chama chetu kwa muda sasa kinao utaratibu wa kuwalipa watu ili wajitokeze kuhamasisha wengine kujitokeza kwenye maandamano.

Hii ni kweli kwenye mikutano ya hadhara pia, ingawa sisi hupenda sana wengi wa wanaojitolea na wapinzani wetu wa CCM wasijue kuwa huwa tunagharimia mambo hayo.

Nakumbuka tukiwa chuo kikuu, mimi nikiwa mwenyekiti wa CHASO DUCE, tulivyokuwa tukilipa makundi ya wanafunzi ili wajitokeze kwenye makongamano ya katiba siku hizo.

Mzee Warioba amewahi kuzomewa na kundi la wanafunzi wanachama wa chadema pale Karimjee hall alipoanza speech yake kwa kusapoti ile orodha iliyoitwa siku zile "sacrosanct issues" hakika tulimzomea. alikatisha hotuba yake. Vilevile, tulikuwa tukiwalipa hela kutoka makao makuu ya chama wanafunzi baadhi ili wahamasishe maandamano na migomo chuoni.

Hivyo basi kwenye mikutano yetu, huwajazia mafuta bodaboda na watu wa bajaji, na katika maandamano huwa wanalipwa baadhi ya watu ili kuhimiza wengine.

Ni kweli hawalipwi wote, lakini hakika kuna wanaokuwa wamelipwa ili kuonyesha kuwa tunaungwa mkono na hao waongoze kuitikia hatimaye wengine wajiunge nao. Kwa hiyo katika maandamano kuna wanaolipwa na kuna wengi wasiolipwa.

Naandika mada hii kuwasadia wale ambao hujitolea tu wajue kuwa katika mkusanyiko huo kuna wenzao ambao huwa wamelipwa hela na hawa wakishawahamasisha wengine wao huishia zao kwahiyo wanaokuja kupatwa na matatizo hasa ni wale wanaojitolea tu bila kulipwa chochote.

Najua kisa kimoja Mbeya, pale waandamanaji walipoumizwa, walijiuguza wao wenyewe bila msaada wa chama. jambo hilo liliumiza sana familia zao na kwa hali ya sasa mbeya na hasa Mwanjelwa lilipotokea tukio lile, vijana hawajitokezi kwenye maandamano, bali wanadai na watoto wa viongozi nao waje mbele ndipo wataandamana. kwa hiyo ndiyo maana pia Mbeya wamegomea maandamano haya ya CHADEMA.

Hatimaye, nawaomba wananchi watafakari kama kila mtu ataachwa kucheza na sheria atakavyo, nini itakuwa future ya nchi yetu!. nina hakika chama chetu cha CHADEMA kikiingia madarakani mwaka 2015 (???) hatutaruhusu maandamano kama haya ya sasa.

Mfano tumeshaonyesha kwa chama kuzuia wanachama wake na mashabiki kuhudhuria mikutano ya Zitto Kabwe. hulka hiyo itakuwa kubwa kwa wapinzani mwaka kesho tutakapochukua dola!

Wenye masikio na wasikie.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni