.

Jumamosi, 6 Septemba 2014

Damu ya Watu Ambao Wamepona Ugonjwa wa Ebola Kutumika Kama Dawa Kuponesha Wengine

Shirika la afya duniani WHO limesema kuwa damu ya watu ambao wameponea ugonjwa wa Ebola inaweza kutumiwa kuwauguza wagonjwa wengine.
 
Katika mkutano mjini Geneva, wataalam wa shirika hilo walikubaliana kwamba hii itakuwa njia ya haraka na ilio salama dhidi ya ugonjwa wa Ebola,sababu kuu ikiwa kwamba kinga ya mwili katika damu ya mtu aliyepona inaweza kukabiliana na virusi hivyo.
Wataalam hao pia wanataka matibabu mengine kuharakishwa ikiwemo dawa ya Zmapp pamoja na chanjo zengine mbili.
EBOLA134
Idadi ya watu wanaodaiwa kufariki kutokana na ugonjwa wa Ebola imepita elfu mbili.
Zaidi ya watu elfu nne wameambukizwa ugonjwa huo huku tiba yake ikiwa bado haijajulikana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni