.

Jumamosi, 21 Septemba 2013

Watu wenye silaha hatari wavamia Westgate Shopping Center Kenya na kuuwa zaidi ya 15 na kujeruhi zaidi ya 50

Watu wanaosemekana kuwa na silaha kali wavamia kituo cha biashara "Westgate Shopping Mall" iliyoko Westland, Nairobi, Kenya, na kufyatua risasi kwa watu waliokuwa katika jengo hilo wakifanya manunuzi ya bidhaa mbalimbali, leo hii mida ya saa 06:50 mchana. idadi iliyothibitishwa ya waliofariki imefikia 11 huku 31 wakiwa wamejeruhiwa, lakini kutokana na shirika la msalaba mwekundu idadi ya waliofariki ni 22 huku zaidi ya 50 wakiwa wamejeruhiwa
Askari tayari wameshalizunguka jengo hilo, na kuokoa idadi kubwa ya watu waliokuwa ndani, huku wavamizi hao wakisemekana kuwepo ndani ya jengo hilo ambalo ni kubwa sana.
yameshapita masaa 7 tangu tukio hilo litokee na bado askari wamelizunguka eneo hilo, ambapo haijulikani kama bado kuna watu waliotekwa na wengine kuendelea kubaki ndani ya jengo hilo, lakini taarifa zikidai kuwa askari wameshalizunguka eneo kubwa la jengo hilo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni