Jumamosi, 21 Septemba 2013
VIDEO QUEEN AGNESS MASOGANGE AACHIWA HURU BAADA YA KULIPA FAINI YA SHILINGI MILIONI 4.8.
Tegemea picha zaidi za ‘asset’ ya Agnes Gerald aka Masogange kwenye Instagram sababu video vixen huyo ni mtu huru kabisa.
Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi la leo, Mahakama ya Kempton ya jijini Johannesburg, nchini Afrika Kusini imemwachia huru mrembo huyo baada ya kulipa faini ya R30,000 ambazo ni sawa na shilingi milioni 4.8 za Tanzania, kubeba kemikali zinazotumika kutengeneza dawa za kulevya.
Naye Melissa Edward ameachiwa huru na mahakama hiyo, baada ya kukosekana ushahidi wowote wa kumtia hatiani.
Habari hiyo kwenye gazeti la Mwananchi inaeleza kwa urefu:
Msemaji wa Kitengo cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai cha Afrika Kusini(Hawk), Kapteni Paul Ramaloko alisema Watanzania hao wameachiwa huru baada ya kuonekana kuwa hawakubeba dawa za kulevya, bali kemikali aina ya ephedrine.
Mahakama hiyo ilibaini kuwa, Melissa hana hatia kwa kuwa ilionekana kuwa amemsindikiza Masogange, ambaye alimwomba amsaidie kubeba mzigo huo.
“Mahakama iliona kuwa Melissa aliombwa tu kumsaidia kubeba baadhi ya mabegi, lakini hayakuwa yake. Mizigo yote iliandikwa jina la Agness Gerald na si Melissa,” gazeti la Mwananchi limemnukuu Kapteni Ramaloko.
Alisema, Melissa alijitetea kuwa hakuwa amesafiri pamoja na Masogange bali walikutana ndani ya ndege na Masogange alimwomba amsaidie kubeba mizigo hiyo, kwani ilikuwa mikubwa.
Kwa sheria za Afrika Kusini kubeba kemikali zozote ambazo zimepigwa marufuku ni kosa la jinai kisheria, hivyo mahakama iliamuru Masogange ahukumiwe kwenda jela kwa miezi 30 (miaka miwili na miezi mitano) au alipe faini ya R30, 000 (sawa na Sh4.8 milioni).
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni