Jumamosi, 21 Septemba 2013
Kuelekea Mechi Ya United Na City, Rooney Anasema Upinzania Wao Umebadilika
Mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney amesema upinzani wa soka baina ya United na Liverpool ume ondoa upinzani mkubwa katika mchezo wa Manchester derby.
Kesho mabingwa hao watetezi wa taji la ligi kuu ya soka nchini England watakuwa wakikabiliana na Manchester City mchezo ambao utapigwa katika dimba la Etihad mchezo ambao unaweza ukawa ni taswira ya kuelekea katika taji mwezi Mei, lakini mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England anaamini kuwa kucheza na Liverpool kunaleta msisimko zaidi.
“City imekuwa na mafanikio hivi karibuni lakini ninaweza kusema kuwa mchezo baina ya United na Liverpool bado ni mchezo mkubwa zaidi.”
Lakini Rooney, ambaye amefunga jumla ya magoli saba katika jumla ya michezo 19 waliyokutana dhidi ya City, yuko makini juu ya umuhimu wa mchezo huo na kwamba watakwenda sambamba na City ambao wanatazamwa sana juu ya nafasi yao ya kutwaa taji.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni