Jumatatu, 30 Septemba 2013
MWANAMKE AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA MITANO JELA BAADA YA KUMTUPA MTOTO WAKE CHOONI
Mwanamke mmoja mkazi wa Manga A Jijini Mbeya amehukumiwa kifungo cha miaka 5 jela kwa kosa la kutupa mtoto wake chooni. Mwaka huu katika eneo hilo baada ya watoto waliokuwa wakicheza kugundua kuwepo kwa Mtoto katika choo cha shimo.
Mtuhumiwa baada ya kukamatwa amekiri kutenda kosa hilo na kwamba alifanya hivyo baada ya mzazi mwenzie kumkataa.
Soma alichosema Solo Thang baada ya kufariki msanii Mack Malik na sikiliza hapa ngoma yao ya zamani “Ndani ya Party”
Msanii Mack Malik ambaye ni mmoja wa wasanii wanaounda kundi la Wateule, amefariki dunia. Mack Malik zaidi ya kuwa producer, pia alikuwa ni rapper. Solothang ameonyesha masikitiko yake kwa kumpoteza Mack Malik, soma maneno aliyoyaandika na sikiliza hapa ngoma yao ya zamani sana akiwa na Solothang. Ngoma hii ni moja kati ya ngoma kali za Solothang na chorus alisimama marehemu Mack Malik
KIJANA ANASWA NA SHEHENA YA BANGI HUKO BUGURUNI..!!
Polisi wakikagua mahali alipokuwa amejificha mtuhumiwa wa bangi.
NJEMBA ACHEZEA KICHAPO CHA MACHANGUDOA BAADA YA KUGOMA KULIPA....!!
WAKATI Oparesheni Fichua Maovu (OFM) inayoendeshwa na Global Publishers ikiwa mzigoni, imenasa tukio la fedheha kwa njemba mmoja akichezea kichapo ‘hevi’ kutoka kwa wanawake waliosadikiwa kuwa machangudoa.
Katika tukio hilo lililojiri hivi karibuni majira ya asubuhi, maeneo ya Afrika Sana jijini Dar, jamaa huyo alidaiwa kuopoa changu ambaye alikwenda kumpa ‘mambo’ ya kiutu uzima kisha wakazinguana.
Mashuhuda wa tukio hilo ambao kwa sehemu kubwa walikuwa ni madada poa, walidai kuwa baada ya jamaa huyo kupewa huduma ya penzi jirani na eneo hilo aligoma kulipa hivyo timbwili zito likaibuka.
UKATILI!! MAMA AMNG'ATA BINTI YAKE SEHEMU ZA SIRI KWA KOSA LA KUJISAIDIA HAJA KUBWA OVYO....
MKAZI wa Kijiji cha Mlongazila, wilayani Kisarawe, Pwani, Moshi Hamad anatuhumiwa kumng’ata mwanaye, Khadija Hamad (6) sehemu za siri kwa madai ya kujisaidia haja kubwa na ndogo hovyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Tanzania Daima juzi wilayani Kisarawe, wakazi hao walisema mama huyo amekuwa na tabia ya kumfungia ndani mtoto wake huyo na kumchapa kwa zaidi ya nusu saa, akitumia nyaya za simu na kumng’ata sehemu mbalimbali za mwili zikiwamo za siri na kumsababishia maumivu makali.
Wakazi hao walisema waliamua kutoa taarifa kwenye dawati la haki za binadamu baada ya kuchoshwa na vitendo hivyo, na sasa wamelitaka Jeshi la Polisi kumkamata mama huyo na kumchukulia hatua.
Stella Musa, alisema sehemu za siri za mtoto huyo zimeharibiwa kutokana na kung’atwa na meno, huku zikiwa na vidonda vinavyodaiwa vimetokana na kuchomwa na kitu chenye ncha kali.
“Wazazi wa mtoto huyo ni wanangu, siku moja mama huyo alimuumiza mkono. Nilimchukua na kukaa naye nyumbani kwangu kwa mwezi mmoja nikimuhudumia kwa kumkanda kwa maji ya moto,” alisema Stella.
Mwalimu wa Shule ya Msingi Mlongazila, Paulo Idana ambaye pia ni katibu wa dawati la kutetea haki za binadamu, alisema suala hilo limewafikia, hivyo wanachukua hatua za kisheria huku mtoto huyo amewekwa chini yao kwa matibabu zaidi.
“Tulimfuata mama huyo Septemba 20 mwaka huu na tulifanya nae mahojiano mbele ya ofisa mtendaji wa kijiji na alikiri akisema alifanya hivyo kwa sababu ya hasira. Tunafanya utaratibu ili tumfikishe kwenye vyombo vya sheria,” alisema Idana.
Akieleza mkasa huo, mtoto huyo alisema wakati mwingine mama yake alikuwa akimwita ili amfundishe kusoma na aliposhindwa aling’atwa mgongoni, mapajani na sehemu za siri huku akisema atamfanyia hivyo hadi ajue kusoma.
Mama wa mtoto huyo, Moshi, alisema alikuwa akitoa adhabu kwa mwanaye huyo kutokana na kujisaidia haja ndogo na kubwa hovyo wakati akirudi shule.
“Nafanya hivi kutokana na hasira siwezi nikamuona mtoto wangu anajisaidia haja kubwa na ndogo kwenye nguo nikamwacha tu, lazima nimwadhibu… jana alitapika kwenye sahani. Je, mtoto kama huyu nitamwacha?” alihoji Moshi.
Mwenyekiti wa kitongoji hicho, Khadija Samizi alikiri kuwepo kwa tukio hilo.
-Tanzania Daima
Jumapili, 29 Septemba 2013
RIPOTI KAMILI YA KIFO CHA DADA WA MWEKITI WA CHADEMA MH. FREEMAN MBOWE ALIYEPINDUKA NA GARI...!!!
DADA wa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amefariki papo hapo baada ya gari alilokuwa akiendesha kupasuka tairi ya mbele na kuingia chini ya daraja baada ya kupinduka na kusababisha watu wawili kufa na wengine watatu kujeruhiwa vibaya.
Dada huyo, Grace Aikaeli Mbowe, anayesadikiwa kuwa na umri kati ya miaka 47 hadi 50, alikuwa akiendesha gari yenye namba T 277 CAJ aina ya Toyota Cresta akiwa na mumewe aliyefahamika kwa jina la Ibrahim Lukindo (52), wakitokea Jijini Tanga, walipata ajali hiyo eneo la Kabuku wilayani Handeni.
Kamanda wa polisi mkoani Tanga (ACP) Costatine Massawe alisema kupitia Ofisa wake wa upelelezi mkoani Tanga, Bw Aziz Kimata, kwamba ajali hiyo ilitokea majira ya saa 1:30 asubuhi jana katika eneo hilo baada ya gari hilo kupasuka tairi ya mbele kulia na kisha kuingia chini ya daraja lililokuwepo eneo hilo.
"Ni kweli kuna ajali ilitokea eneo la Kabuku gari aina ya Cresta lililokuwa likiendeshwa na ndugu inavyosemekana wa Bw Freeman Mbowe, limepata ajali baada ya kupasuka tairi la mbele na kuacha barabara na kuingia chini ya daraja .
"Dereva anayeitwa Grace Aikael Mbowe na mtu anayesemekana ni mumewe anayeitwa Ibrahim Lukindo, wamefariki na watu watatu waliowachukua wamejeruhiwa," alisema RCO Kimata.
Aliwataja waliojeruhiwa kuwa ni pamoja na Bw Ridhiwani Bakari (29) aliyekuwa na mkewe Zeddy Nzuke (29) raia wa Kenya aliyekuwa na mtoto wake mwenye umri wa miaka miwili na miezi minne aliyefahamika kwa jina la Mariam Ridhiwan ambao kwa sasa wamelazwa katika hospitali ya Magunga wilayani Korogwe.
RCO Kimata aliyezungumza kwa niaba ya kamanda huyo wa polisi alisema chanzo cha ajali hiyo inasemekana kimetokana na kupasuka kwa mpira huo na mwendo kasi wa kawaida na kwamba majeruhi na maiti zi9mehifadhiwa kwenye hospitali hiyo.
Mwandishi wa habari hizi, aliyefika kwenye hospitali hiyo na kuzungumza na Ridhiwani pamja na mkewe ambaye amelazwa wodi namba mbili ya wanawake katika hospitali hiyo, alisema kwamba ndoto zake za kufanya kazi Dar es salaam zimezimika ghafla kutokana na kwamba alikuwa aende kupamba kazi ya uofisa ugavi katika taasisi moja ya fedha ya marehemu Mbowe Jijini Dar es salaam.
"Nilikuwa naenda kupewa kazi na mama Mbowe katika Institution yake ya Micro-Financial Jijini Dar es salaam, mimi ni procurement (Mgavi-manunuzi) na ni Mkenya kwetu ni Eastern Province Kang'undo na nimeolewa na bwana Mtizedi...Lakini sasa ndoto zangu za kufanya kazi Dar es salaam zimezimika ghafla," alisema Zeddy akiwa kitandani amelala na mwanwe ambaye alikuwa haongei tangu amefika katika hospitalini hapo.
Mumewe na mwanamke huyo akizungumzia ajali hiyo alisema kuwa hakuwa akijua kwani alikuwa amelala dakika tatu kabla ya kutokea ajali hiyo ambapo alishtukia yeye, mkewe na mwanawe wametupwa chini kwenye majani wakiwa hawajijui na walikimbizwa katika hospitali hiyo ya Korogwe
Ridhin ambaye ni mkazi wa Nguvumali Jijini Tanga, alisema safari yao hiyo ilikuwa ifanyike Jumamosi mchana lakini kutokana na na kuchelewa kwa wenyeji wao hao, waliondoka Tanga kwenye hoteli ya Doliphin walikolala majira ya saa 11:00 alifajiri kwa ajili ya kwenda Jijini Dar es salaam.
Muuguzi wa zamu wa hospitali hiyo Bi Nayela Missingo alikiri kuwapokea wagonjwa hao ambapo alisema wanafanya jitihada za kuwahamishia katika hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam mtoto Mariam ambaye amepata majeraha katika kichwa chake na kwamba tangu afikishe hospilaini hapo hakuwa katika hali nzuri, haongei walakunyonya.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)