Ukraine, Georgia na Moldova zimetia sahihi mikataba ya ushirikiano na muungano wa ulaya, swala ambalo Urusi inapinga vikali.
Makubaliano hayo ambayo yatayaunganisha pamoja
mataifa hayo na kuyaegemeza Magharibi kiuchumi na kisiasa, haswa ndio
msingi wa mgogoro ulioko Ukraine.Usitishaji wa vita kati ya vikosi vya serikali na waasi wanaounga mkono Urusi, mashariki mwa Ukraine, unakamilika Ijumaa hii.
Rais wa Ukraine, Petro Poroshenko aliusifu mkataba huo akisema ni siku ya kihistoria katika taifa la Ukraine baada ya siku ya Uhuru wa taifa hilo mwaka 1991.
Ameutaja kuwa dalili ya imani na nia isiyoweza kuvunjwa.
Kwengineko, rais wa Umoja wa bara Uropa, Herman va Rompuy ametaja kuwa "siku kuu kwa bara Uropa".
''Umoja wa bara Uropa unasimama pamoja nanyi, leo zaidi ya siku nyingine yoyote awali" aliwaambia viongozi wa nchi hizo tatu, akiongeza kuwa hakuna chochote katika mikataba hiyo ya makubaliano kitakachoiletea madhara Urusi kwa njia yoyote ile.
Naibu waziri wa maswala ya nje wa Urusi, Grigory Karasin ''ameliambia shirika la habari la Interfax kuwa hatua hiyo huenda ikazua madhara.
Kutiwa sahihi kwa mkataba huu muhimu, kwa hakika ni haki ya taifa lolote lile" alisema.
Ila tu matokeo ya Ukraine na Moldova kutia saini mkataba huu bila shaka yatakuwa mabaya".
Mapema, mshauri mkuu wa Kremlin, Sergei Glazyev alimtaja Poroshenko kuwa mwanachama wa Nazi na kuwa uchaguzi wake kuwa rais haukuwa wa haki kwani sehemu kubwa ya Ukraine haikupiga kura katika uchaguzi wa mwezi Mei.
Alizidi kusema kuwa Poroshenko hana haki kikatiba kutia sahihi mkataba huo, jambo ambalo litadhuru uchumi wa Ukraine
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni