Watu
wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha ya bunduki aina
ya SMG na bastola waliokuwa wakitumia pikipiki aina ya sanlg yenye namba
T460 CVQ wamevamia duka la mpesa na kumuua mfanyabiashara Gosbert
Kulwa(59) mkazi wa tambukaleli mjini Geita.
Kamanda
wa polisi mkoani Geita Joseph Konyo amesema tukio hilo limetokea jana
majira ya saa 11.30 jioni katika eneo la benki ya NMB ambapo majambazi
hao walimpiga risasi ya tumboni mfanyabiashara huyo wa mpesa na kufariki
dunia wakati akipata matibabu katika hospitali ya wilaya ya Geita.
Amesema
mauaji hayo yalifanyika baada ya majambazi hao kupora kiasi cha pesa
ambacho hakijajulikana kutoka kwa mfanyabiashara huyo.
Kamanda
ameongeza kuwa kabla hawajamuua Gosbert walianzia kwenye duka la
mfanyabiashara wa vinywaji ndugu Ignas Athanas na walichukua pesa kiasi
ambacho hakijafahamika na kuchukua bastola aina ya H PIETRO BERRETA HO4788Y CAR 5808 ikiwa na risasi 12 mali ya mfanyabiashara huyo.
Aidha
majambazi hao waliokuwa na bunduki aina ya SMG iliyofutwa namba zake na
risasi 13 na simu ya mkononi aina ya TECNO huku wakiwa wamevalia makoti
meusi na helment ili kuficha sura zao zisitambulike kwa urahisi.
Jeshi
la polisi lilipata taarifa muda mfupi zilizotolewa na raia wema ambapo
kamanda wa polisi akiongoza kuwafuatilia majambazi hao walifanikiwa
kuwakuta katika pori lililopo jirani na kijiji cha Ibambila wilayani
Nyangh’hwale zaidi ya km 50 kutoka mjini Geita walipofanya uharifu.
Wakiwa wanakimbizana majambazi hao walipowaona askari jambazi mmoja aliyekuwa na silaha aliruka kwenye pikipiki na kuanza kuwashambulia
askari kwa risasi lakini dereva wa porisi alimfuta moja kwa moja na
kumgonga kwa gari jambazi huyo na kufariki hapo hapo.
Baada
ya hapo jambazi mwingine alikimbia kwa pikipiki na askari wakaanza
kumfukuza wakishirikiana na wanafunzi wa shule ya sekondari Nyang’hwale
na kufanikiwa kumkamata na kuanza kumshambulia na alifariki wakati
anakimbizwa kupelekwa hospitali.
Taharuki
hiyo iliyokuwa imeikumba mji wa Geita kwa masaa takribani 3 kabala
hawajakamatwa majira ya saa2 baadhi ya wananchi wamelipongeza jeshi la
polisi kwa kazi waliyoifanya kwa mda mfupi mara baada ya tukio hilo huku
kamanda Konyo akiendelea kuwaasa wananchi wazidi kutoa ushirikiano kwa
jeshi la polisi ili kuimarisha amani katika mkoa huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni