.

Jumanne, 2 Septemba 2014

Marekani yashambulia mtandao wa al-Shabaab


Image
Kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya ulinzi wa Marekani, Pentagon, shambulizi hilo lilikuwa likimlenga kiongozi aliyekuwa mafichoni wa mtandao huo. Msemaji wa Pentagon, John Kirb, amesema Marekani inafuatilia matokeo yake na itatoa maelezo zaidi pale taarifa itakapopatikana. Hata hivyo hakukuwa na taarifa zaidi zilizoweza kupatikana.
Afisa mwandamizi wa usalama nchini Somalia alisema ndege inayoruka bila ya rubani ilimlenga kiongozi wa al-Shabaab Ahmed Abdi Godane, muda mfupi baada ya kuondoka katika mkutano wa viongozi wa mtandao huo. Godane ambaye anajulikana pia kama Mukhtar Abu Zubeyr ni kiongozi wa kidini wa kundi hilo lenye mafungamano na mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda.
Tetesi za kuuwawa Godane
Afisa mmoja wa Somalia aliyeongea pasipo kutaja jina lake kutokana na kutokuwa na mamlaka ya kufanya hivyo, amesema taarifa za uchunguzi zinaonesha anaweza kuwa ameuwawa sambamba na wapiganaji wengine. Taarifa zinaeleza kuwa shambulizi hilo limefanyika katika msitu mmoja ulio karibu na wilaya ya Sablale, umbali wa kilometa 170, kusini mwa Mogadishu, eneo ambalo al-Shabaab inalitumia kutoa mafunzo kwa wapiganaji wake.
Gavana wa jimbo la Lower Shabelle nchini Somalia, Abdiqadir Mohammed Nor, aliliambia shirika la habari la AP kwamba majeshi ya serikali na Umoja wa Afrika wanaelekea mji wa Sablale na kwamba walisikia mzizimo kama wa tetemeko la ardhi wakati ndege zinazoruka bila rubani zilipoishambulia kambi ya al Shabaab.
Mlolongo wa mashambulizi ya Marekani nchini Somalia
Marekani imekuwa ikifanya mashambulizi ya angani nchini Somalia katika miaka ya hivi karibuni. Shambulizi lake la kombora lake la mwezi Januari liliweza kumua afisia wa ngazi wa juu kabisa katika masuala ya usalama wa al Shabaab na mwezi wa kumi mwaka uliyopita gari iliyokuwa imebeba wanachama wa kundi hilo ilishambuliwa na kusababisha kifo cha mtaalamu wa juu kabisa wa viripuzi wa mtandao huo.
Hatua hii ya sasa ya Marekani kinatokea baada ya majeshi ya serikali ya Somalia kufanikiwa kulirejesha katika udhibiti wake gereza kubwa mjini Mogadishu, ambalo lilishambuliwa na watu saba wenye silaha nzito, ambao wanahisiwa kuwa wanamgambo, walikuwa katika jaribio la kutaka kuwaachia huru wenzao wengine wenye itikadi kali ambao wamefungwa. Hata hivyo taarifa ya Pentagon haijaeleza kama shambulizi hili linahusiana na lile la gerzani au la.
Maafisa nchini Somalia wanasema washambuliaji wote sana, wanajeshi watatu wa serikali na raia wawili waliuwawa. Gereza la Godka Jilacow la mijini Mogadishu ni kituo mahojiano cha idara ya upelezi ya Somalia ambapo kunaelezwa kuwepo kwa wafungwa kutoka kundi la al-Shabaab ambao wanashikiliwa chini ya ardhi.

NATAFUTA MWANAUME KIDUME, ANAYEWEZA MAMBO"......KAMA UNAMTAKA HUYU INGIA HAPA -


http://yamotto.blogspot.com/2014/08/natafuta-mwanaume-kidume-anayeweza.html  
Naitwa Debora, ninahitaji mwanaume rijali kweli kama unataka naomba angalia picha hizi zangu hapa, then tuwasiliane -

Jumatatu, 1 Septemba 2014

Diamond aokolewa na polisi Ujerumani

Usiku wa Jumamosi Agosti 30, 2014, majira ya saa 10 alfajiri, mwanamuziki nyota wa Bongo Flavor, Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platnumz alijikuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart, Ujerumani, baada ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show.

Sehemu ya ukumbi ulioharibiwa vibaya na washabiki mjini Stuttgart, Ujerumani.
Sehemu ya ukumbi ulioharibiwa vibaya na washabiki mjini Stuttgart, Ujerumani.
Mashabiki hao waliokuwa wamelipa tiketi euro 25 kwa kiingilio walihadiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku, lakini walijukuta wakisubiri hadi majira ya saa 10 alfajiri ndipo mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake raia wa Nigeria anayejiita Britts Event.
Hapo ndipo washabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki Diamond na promota wake, Kilichowakera zaidi washabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya mashabiki kuvunja hadi vyombo vya muziki, ma-Djs walishambuliwa na wapo hospitalini kwa sasa.
Mmoja wa Djs hao alipoteza lap top yake, mwanadada DJ Flor alipatwa mstuko wa moyo na kukimbizwa hospitali, washabiki hao walimpa kipigo DJ Drazee naye yupo hoi hospitali. Polisi nchini Ujerumani wanamesema tukio hili la aibu halijawahi kutokea, kuwa msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa Ujerumani ni kitu cha hatari kwani washabiki wa Ujerumani wanaheshimu sana muda wao.
Diamond Platnumz akiwapagawisha mashabiki wake katika moja ya maonyesho yake.
Diamond Platnumz akiwapagawisha mashabiki wake katika moja ya maonyesho yake.
Mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onyesho hilo na wamesema wanachunguza thamani ya hasara iliyosababishwa na ghasia hizo na pia itamfungulia mashataka promota huyo raia wa Nigeria ambaye pia anachunguzwa kwa kujihusisha na mtandao fulani wa biashara.
Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti hii…
http://www.stuttgarter-nachrichten.de/inhalt.blaulicht-aus-der-region-stuttgart-31-august-diamond-platnumz-zieht-aerger-der-fans-auf-sich.ca1f4b9d-599b-4c95-84c8-fe25d10b6ed9.html

Shilole akiri kutotumia Condom kwenye mapenzi


Mwigizaji  wa  filamu  na  mwanamuziki  wa  miondoko    ya  kizazi  kipya, Zuwena  Mohammed  ‘Sholole’  amesema  kuwa  matumizi  ya  kondom  wakati  wa  mahaba  hayaleti  ladha  ndio  maana   alilazimika  kwenda  kupima  ngoma  na  mpenzi  wake  Nuh  Mziwanda  ili  wasiwe  wanatumia  kondom.
nuhu
 
Akizungumza  na  Mpekuzi  wetu, Shilole  alisema  kuwa  raha  ya  mapenzi  ni  kila  mmoja  kuwa  na  mwenzake  bila  kuwa  na  kizuizi  chenya  kuondoa  ladha  hiyo  na  baada  ya  kupima  kila  mmoja  ameapa  kutochepuka  ili  asilite  maambukizi  ndani  ya  uhusiano  wao….
SHILOLE
 
“Asikudanganye  mtu, raha  ya  kula  ndizi  ni  kula  ikiwa  imemenywa, ikiwa  na  maganda  inaondoa  utamu  ndio  maaa  mimi  na  mwenzangu  tulilazimika  kwenda  kupima  afya  zetu  na  kila  mmoja  alibainika  ni  mzima hivyo  tumeahidiana  kutosalitiana  ili  tusileteane  maambukizi”,alisea  Shilole.

Jeuri ya Pesa: KAJALA sasa kumwajiri WEMA SEPETU

AMA kweli fedha mwanaharamu! Kama bado ulikuwa ukiamini kwamba Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu anayependelea kuitwa Madam ana mtonyo (fedha) kumzidi aliyekuwa shosti wake, mwigizaji Kajala Masanja ‘Kay’, umekosea sana kwani upepo umegeuka.
 
Habari za ‘ufukunyuku’ zinadai kwamba, kwa utajiri alionao kwa sasa, Kajala anaweza kudiriki kumwajiri Wema kama kisemavyo chanzo.
 
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na wote kwa maana ya kutafuna pande zote, mwigizaji huyo ambaye enzi za ushosti wake na Wema alikuwa akionekana kama kijakazi, sasa fedha imemtembelea kiasi cha kutosha wakati mwenzake kwa bahati mbaya eti ‘anatembelea ringi’.
 
Chanzo kilisema kwamba Kajala kwa sasa ana maisha ya ‘kitonga’, amepanga kwenye nyumba nzuri ya ghorofa, ana kampuni yake ya filamu (KAY Entertainment), magari manne, anatembea na wapambe (walinzi) huku akaunti yake benki ikiwa imetuna.
Nyota wa muvi za Kibongo, Kajala Masanja Akiwa na WEMA
Nyota wa muvi za Kibongo, Kajala Masanja Akiwa na WEMA
 
“Kajala ameonesha jeuri ya fedha. Ametoka katika nyumba ya kawaida sasa analala angani. Kwa taarifa yenu amepanga ghorofa nzima maeneo ya Sinza-Madukani jijini Dar.
 
“Yupo vizuri, anamiliki ofisi kubwa ya kuzalisha sinema, magari mawili ya ofisi pamoja na magari mawili ya kutembelea (Brevis na Harrier) na anaishi katika nyumba anayolipa kodi kwa mwezi dola 2,000 (zaidi ya Sh. milioni 3.2),” kilidai chanzo hicho na kudai kwamba si mbaya Kajala akamkumbuka mwenzake hata kwa kumwajiri kwenye kampuni yake.
 
KAJALA AMEHONGWA?
Akizungumza na waandishi wetu, Kajala alisema anamshukuru Mungu kwani fedha hizo amezizalisha kupitia kazi zake pamoja na biashara mbalimbali alizokuwa akizifanya, hajahongwa na mtu yeyote.
 
“Sijahongwa na mtu yeyote, kila mtu ana akili zake katika kutafuta fedha, nafanya biashara huku nikiigiza sinema zangu na Mungu amenijalia mambo yanakwenda vizuri,” alisema Kajala.
 
Kuhusu kumwajiri staa mwezake huyo, Kajala hakutaka kulizungumzia hilo.
 
WEMA HALI IPOJE?
Utafiti uliofanywa na Ijumaa Wikienda umebaini kwamba Wema aliyemlipia Kajala Sh. milioni 13 asiende jela mwaka jana, ambaye kipindi kifupi kilichopita alikuwa na kampuni ya kuzalisha sinema, wapambe, akaunti iliyonona benki, magari ya kifahari ya kutembelea na samani nyingine, nyingi zimepotea kama si kuyeyuka kabisa.
Gari la aina ya Toyota Brevis inayomilikiwa na Kajala.
Utafiti umeonesha Wema ambaye alikuwa akimiliki magari kadhaa likiwemo la kufanyia kazi za sinema, kwa sasa amebakiwa na gari moja tu ambalo ni Toyota Harrier. 
 
Kama hiyo haitoshi, ilidaiwa kuwa hata akaunti benki haijanona na hata wapambe wa kutembea naye wameyeyuka.
 
WEMA ATAFUTWA
Ili kutaka kujua anazungumziaje ‘challenge’ hiyo ya kudaiwa kuporomoka kiuchumi, wanahabari wetu walimtafuta Wema kwa siku tatu mfululizo lakini hakupatikana huku simu yake ikiita muda mrefu bila kupokelewa.
 
SHOSTI WAKE
Akizungumza na waandishi wetu kwa sharti la kutoanika jina , rafiki wa karibu wa Wema alikiri kuwa staa huyo mwenye nyota isiyochuja, ameshuka kiuchumi tofauti na enzi zile ambazo walikuwa wakitanua katika viunga mbalimbali na msururu wa watu huku Madam akisimamia shoo nzima ya malipo.
 
“Madam kwa sasa ameshuka kiuchumi kwani hatutanui mjini kama ilivyokuwa zamani, yaani naamini anaweza kuajiriwa na Kajala ambaye wakati ule alikuwa chini kwake,” alisema rafiki huyo.
KUMBUKUMBU YA JUZIKATI
Hivi karibuni, baadhi ya mashabiki wa Wema ambao wanajiita Team Wema, walimuonya staa wao huyo wakidai ananyonywa na mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye pia amekuwa akimdhalilisha katika majukwaa pindi anapofanya shoo zake.
 
Walimtaka abadilike kwani yeye ndiye mwenye nyota ya kung’aa lakini Diamond ananufaika yeye peke yake na muziki wake.
 
DIAMOND ALINENA
Baada ya Diamond kushambuliwa na Team Wema, naye alitoa majibu ambayo yalionesha dhahiri kwamba ndiyo sababu inayomfanya Wema ashuke kisanaa na kiuchumi.
 
“Kama kweli mnampenda huyo msanii wenu (Wema) basi mngemshauri kwanza akaacha kufanya starehe kuliko kuelekeza lawama kwangu, mimi kama mume, jukumu langu ni kuhakikisha namwezesha kuanzisha biashara lakini jukumu la kuendeleza ni la kwake, mnataka hata kuigiza nikamuigizie?,” alihoji Diamond mtandaoni.
Tupe maoni yako hapo Chini..!!

Gari lateketea kwa moto mkoani Morogoro



moto
GARI dogo ambalo halikupatikana namba zake limeteketea kwa moto leo maeneo ya Msamvu mkoani Morogoro. Mpaka mpigapicha hizi akiondoka eneo la tukio, chanzo cha moto huo kilikuwa bado hakijafahamika.
 

Tupe maoni yako hapo Chini..!!

Boko Haram 70 wauawa .



wanajeshi wa serikali ya Nigeria.
Jeshi la Nigeria limetoa ripopoti kua mpaka sasa limekwisha waua wapiganaji 70 kutoka katika kikundi cha kiislam cha BOKO HARAM,kutokana na mashambulizi kati ya kikundi hicho na wanajeshi wa Nigeria kaskazini -mashariki mwa mji wa Bama.
Boko Haram walifika mapema asubuhi katika mji huo wakiwa na magari ya kivita,taarifa kutoka katika mji huo zinaeleza kwamba mashambulizi yalianzishwa na vikosi vya jeshi la Nigeria.
Msemaji wa kundi hilo la Boko Haram ameelezea hali ya mji huo kwa sasa kua wakaazi wa mji wa Bama wamekimbilia katika mji mwingine wa Borno na Maiduguri .
Nalo shirika la Amnest International limetoa takwimu raia wapatao milioni nne wamekufa mwaka huu katika mgogoro huo kati ya Boko Haram na vikosi vya ulinzi vya Nigeria.