Jumatano, 5 Februari 2014
TAARIFA YA KUKATIKA KWA MAWASILIANO YA VODACOM
Dar es Salaam, 5 Februari, 2014.Tunapenda kuwaomba radhi wateja wetu wote kwa kushindwa kutoa huduma za mawasiliano kuanzia asubuhi ya Februari 5, 2014. Hii imetokana na kukatika kwa mkonga wa mawasiliano ulioko barabara ya Morogoro na nyingine mbili za ziada zilizoko Mlalakuwa na Mayfair plaza barabara ya Mwai kibaki jijini Dar es Salaam.
Kukatika kwa Mkonga huo kumesababisha vituo vyetu vya kutoa huduma za mawasiliano vilivyopo Oysterbay na mbezi juu kushindwa kufanya kazi kutokana na vituo hivyo kutegemeana kumesababisha kushindwa kutoa huduma za mawasiliano.
Kutokana na hilo wateja hawakuwa na uwezo wa kupiga simu, kutumia intaneti na hata huduma za kifedha. Tunatambua usumbufu ambao umetokea kwa kukosa mawasiliano, kwa mara nyingine tena tunaomba radhi na tunashukuru kwa uvumilivu wao katika kipindi chote ambacho huduma zilikosekana.
Mafundi wetu wameweza kurekebisha uharibifu uliotokea barabara ya Mwai kibaki ambao uliotokana na shughuli za ujenzi wa barabara zinazoendelea. Uharibifu mwingine uliotokea katika Barabara ya Mlalakuwa ulichukua muda kurekebisha kutokana na nyaya zilizo katika mkonga wa mawasiliano kuungua kulikosababishwa na zoezi la uchomaji taka lililokuwa linaendelea katika sehemu ambayo mkongo umepita na kusababisha uharibifu huo.
Napenda kuwahakikishia wateja wetu kuwa, Tumejidhatiti katika kuendelea kutoa huduma bora na za kipekee wakati wote watakapokuwa wanautumia mtandao wa Vodacom, Tunawashukuru kwa namna ambavyo wameendelea kutuunga mkono na kutuvumilia pale matatizo yanapojitokeza.
Rene Meza
Mkurugenzi Mtendaji – Vodacom Tanzania
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni