![Screen Shot 2014-02-08 at 12.35.39 PM](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_vfuHVIRSXYdQVXvVXNqPXZ6EhpiUye5nTyC77ERQFyleiXimAg0j2YjyUkfnH_E12HpvQzCi2MqlvlN8qQsauriCHyLE4OM0QbqgMgQF-v3TSYM0r8m_BGi2WYbVjMoww3G2gZCQxl91wIrgChxjwy4ASK8nNbCk_E21YkFbH47Ld4WyPvB9X9aLXv4diHVALbG6KZR2k=s0-d)
Unaweza
kujaribu kutengeneza picha, pale ambapo msanii anaamua kushika bunduki
na kuingia kwenye vita ya nchi yake kisa hajapendezwa na upande mmoja
kati ya mbili zinazopingana.
Imeripotiwa kwamba huenda aliewahi kuwa mshiriki wa shindano la
Tusker Project fame Kuonck ‘K-Denk’ Deng na kuiwakilisha nchi yake ya
Sudan ya Kusini, ameamua kushika silaha na kuingia vitani.
![Screen Shot 2014-02-08 at 12.20.59 PM](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_slqWcQdLURziArUJnYMJd1k4aXeaZYRFVAMozAtjkiL3ooWUHcwi4l2KpextZw4xPid3PjXSsJCiqXRSrSkjZQmSaiviR9KYW3_Fk64S8q4BcTrU5gfcvXzIIzSWcjSkKVG9RtXl6Z62aN5_rm9ftbiXhmtoOQKJWI-_hgNSlQGh-ZkEUcz82tMVNxNqSwuRhxAX51zg=s0-d)
Kwenye
page yake ya facebook, K Denk amepost status kadhaa zenye utata ambazo
mapokezi yake hayajawa mazuri… na hii imeonekana toka vita ianze
December 2013 nyumbani kwao Sudan.
Updates zinaonyesha msanii huyu alieamua kuingia vitani, amehama
kutoka Juba hadi sehemu ya kaskazini ambayo inashikiliwa na Waasi.
![Screen Shot 2014-02-08 at 12.25.01 PM](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_snu5S3r4AaiSqyE1KFVayM6Sq6HyvgWix_3IF6TyUGFcLf2yD4Qp95Ti5n0IsR5UkXVdqTTw3rYBflySnXWmVumO1G9dU5BTN39IhI9M7ij_Y7PKSAeY_UMlWT2aad2V6Daa6Wx66Dw2qHuKoCysAiWrvnIrnwognPfFqs66xPojjWuFG5T-yoTpuNFWZGW3AXZfeRNzw=s0-d)
K
Denk ameonekana kuwa upande wa Waasi wanaopigana na Serikali huku
akisisitiza kwamba amani itapatikana baada ya Rais Salva Kiir kuuwawa.
Baadhi ya mashabiki zake ambao ni sehemu ya waliopoteza ndugu zao kwenye vita hii hawajasita kumuandikia ya moyoni.
![Screen Shot 2014-02-08 at 12.25.28 PM](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_stWTOBrkBWu-_dO5MvfpeCvZFMCKpjO6sL6VALMChUHAquzoe8dh2MQvwO5jpfMsh9Rivn0ROj9Vh0bTGJKMDONbZs0MXwBKF8m1JOmWQbehzM33yFXiQM9qfrVYffLQaripPatYTfUHNp8DFAzttBdOvtctjKSgPPh9_K3gH0oASmNdcbtRjgj0eq497N75sRdU85CA=s0-d)
Source: gazeti la Daily Nation.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni