Jumamosi, 8 Februari 2014
Msanii wa Project fame alieingia kwenye vita ya nchi, anasema Rais akiuwawa amani ndio itakuja.
Unaweza kujaribu kutengeneza picha, pale ambapo msanii anaamua kushika bunduki na kuingia kwenye vita ya nchi yake kisa hajapendezwa na upande mmoja kati ya mbili zinazopingana.
Imeripotiwa kwamba huenda aliewahi kuwa mshiriki wa shindano la Tusker Project fame Kuonck ‘K-Denk’ Deng na kuiwakilisha nchi yake ya Sudan ya Kusini, ameamua kushika silaha na kuingia vitani.
Kwenye page yake ya facebook, K Denk amepost status kadhaa zenye utata ambazo mapokezi yake hayajawa mazuri… na hii imeonekana toka vita ianze December 2013 nyumbani kwao Sudan.
Updates zinaonyesha msanii huyu alieamua kuingia vitani, amehama kutoka Juba hadi sehemu ya kaskazini ambayo inashikiliwa na Waasi.
K Denk ameonekana kuwa upande wa Waasi wanaopigana na Serikali huku akisisitiza kwamba amani itapatikana baada ya Rais Salva Kiir kuuwawa.
Baadhi ya mashabiki zake ambao ni sehemu ya waliopoteza ndugu zao kwenye vita hii hawajasita kumuandikia ya moyoni.
Source: gazeti la Daily Nation.
MWANAMKE MUIMBA KWAYA MSOMI WA CHUO KIKUU ANASWA AKIJIUZA, AHAHA MCHUNGAJI ASIJUE:
Ni
aibu iliyoje? Mwanadada ambaye amejitambulisha kuwa ni msomi wa chuo
kikuu (jina lipo) ambaye pia ni mwanakwaya chuoni hapo aliyejitaja kwa
jina moja la Rei ameaibika baada ya kunaswa usiku mnene akijiuza, Risasi Jumamosi linaifumua.
Mwanakwaya,msomi wa chuo kikuu (katikati), aliyejitaja kwa jina moja la Rei.
Rei alikamatwa katika msako wa polisi katikati ya Jiji la Dar (City
Center) hivi karibuni akiwa na kundi la warembo wa vyuo mbalimbali
wakifanya biashara haramu ya kuuza miili.
Mrembo huyo ambaye Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers
ilimshuhudia, kabla ya kupelekwa kituo kikuu cha polisi, Wilaya ya
Ilala (Central), alijitetea kuwa yeye ni denti wa chuo kikuu hivyo
kitendo cha kupigwa picha alijua kabisa kuwa zitasambaa mitandaoni hivyo
itakuwa ni aibu kubwa.
“Kaka naomba usinitoe gazetini au mitandaoni, haya ni maisha tu, itakuwa aibu kwa wanachuo wenzangu,” alijitetea.
Mbali na hayo, mrembo huyo wa haja alikuwa akihaha kuwa kama ishu
hiyo itamfikia mchungaji wake, basi hatakuwa na sehemu ya kuficha uso
wake.
Pia Rei alijitetea kuwa huwa hajiuzi kila siku na hiyo ilitokea tu kwa bahati mbaya kwani ana biashara zake binafsi.
Alipoulizwa na ‘kachero’ wetu juu ya kanisa au kwaya anayoitumikia alikataa kutaja kwa madai kuwa atalichafua kanisa.
“Wewe ujue tu mimi ni mwanakwaya, hayo mambo ya kwaya na kanisa sitaki kulichafua jina la Mungu,” alisema.
Mwanakwaya,msomi wa chuo kikuu (katikati).
Kwa mujibu wa polisi wa doria waliowanasa warembo hao walidai kuwa
Jumatano iliyopita watafikishwa katika Mahakama ya Jiji la Dar (Sokoine
Drive) chini ya Hakimu Mkazi, Timothy Lyon kwa kosa la uzururaji kwa
kuwa hakuna sheria ya moja kwa moja juu ya ukahaba.
PICHA MBALI MBALI ZA NICK MINAJ AKIWA BILA WIGI...SHE IS CUTE I LIKE HER LIKE THIS
Jionee Mwenye Mtoto Alivyo Bomba ...Hapo kaweka Usela wote pembeni na yale mawigi yake ya kishetani pembeni ...mtoto unywele Anao ...Dahhhh She is Cute ......
Check picha alafu ucomment
AY AKANUSHA KUMTUNGIA NYIMBO JAGUAR...APINGA KUWA DIAMOND NI TISHIO KWAKE
Msanii wa HipHop kutoka Tanzania, Ambwene Yesaya amekanusha uvumi uliokuwa umezagaa nchini Kenya wa kumuandikia baadhi ya nyimbo mkali wa Kioo kutoka Kenya, Jaguar.
Katika mahojiano aliyofanyiwa nchini Kenya alikokuwa ameenda hivi karibuni, AY amesema hajawai kumuandikia wimbo wowote Jaguar na hata wimbo wao ‘Nimetoka Mbali’ kila mtu aliandika mashairi yake.
“Jaguar ni mmoja wa marafiki zangu. Tumefanya kazi pamoja na hakuna ukweli wowote kuhusiana na tetesi za mimi kumuandikia mashairi ukizingatia amekuwepo kwa muda mrefu kwenye gemu ya muziki hivyo kumfanya kuwa miongoni mwa wasanii wenye uzoefu wa kutosha na kufanya vizuri hata ukitazama ngoma niliyowahi kufanya nae ya Nimetoka Mbali, kila mmoja wetu aliandika mashairi yake kivyake hivyo huna haja ya kubisha kwa uwezo mkubwa alionao na naamini ni ushahidi tosha,” alisema.
Pia AY amepinga muziki wake kuathiriwa na Diamond kwakuwa kila mtu ana malengo yake katika muziki wake.
“Kila msanii ana mipango na mikakati yake ya kufikia malengo aliyojiwekea, sipo kujilinganisha na mtu yoyote, ushindani wangu ni kwa yule anayetaka kujaribu kutengeneza mkwanja mkubwa kushinda wangu, huo ndio ushindani wa kweli, hata hivyo siwezi kuwa juu milele.”
Source:Bongo5
Hawa ndio walioteuliwa kuwa wajumbe wa Bunge maalum la Katiba.
Jioni ya February 07 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Mh.Florence Turuka alitangaza majina ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba,ambalo bunge hilo litakutana kwa siku 70 na kuongezewa 20 kama hawatoafikiana.
Bunge hilo la Katiba litakuwa na jumla ya wajumbe 640 kujadili Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba Desemba 30 2013 majina hayo yalitangazwa kupitia ukumbi wa mikutano wa ofisi za Mawasiliano Ikulu jijini Dar es Salaam.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UTEUZI WA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBAUTANGULIZI
1. Uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba Unatawaliwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura, 83 (The Constitutional Review Act, Cap 83). Sheria hii inaweka mamlaka ya uteuzi, masharti, taratibu, vigezo na mambo mengine yote yanayopaswa kuzingatiwa katika uteuzi wa Wajumbe wa Bunge la Katiba. Kwa mujibu wa Kifungu cha 22 (2A) na (2B) vigezo hivi vinajumuisha umri, jinsia, uzoefu, sifa na mahali anapotoka mjumbe husika.
- Sheria hii inatamka aina tatu za Wajumbe wa Bunge la Katiba kama ifuatavyo:-
(i) Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano;
(ii) Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar; na
(iii) Wajumbe 201 kwa mujibu wa Kifungu Na. 22(1c) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ambayo inaonyesha makundi mbalimbali 10 yanayohusika. -
Makundi hayo ni kama ifuatavyo:-
(ii) Taasisi za Kidini (20)
(iii) Vyama vyote vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu (42);
(iv) Taasisi za Elimu (20);
(v) Watu wenye Ulemavu (20);
(vi) Vyama vya Wafanyakazi (19);
(vii) Vyama vinavyowakilisha Wafugaji (10);
(viii) Vyama vinavyowakilisha wavuvi (10);
(ix) Vyama vya Wakulima (20); na
(x) Vikundi vya Watu wenye Malengo yanayofanana (20).
- Mchakato wa uteuzi ulianza kwa kutoa Tangazo la Mwaliko katika Gazeti la Serikali, Tangazo la Serikali Na 443 la tarehe 13 Desemba, 2013. Tangazo hilo lilitolewa kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza ili kuyaalika makundi yaliyotajwa kisheria kuwasilisha mapendekezo ya majina kwa ajili ya uteuzi katika Bunge laMaalum la Katiba. Aidha, Tangazo hilo la mwaliko lilitangazwa pia katika magazeti mbalimbali yanayosomwa hapa nchini. Pamoja na mambo mengine Tangazo la Mwaliko lilitamka ukomo wa muda wa Taasisi na Makundi kuwasilisha mapendekezo ya majina ya wajumbe kuwa ni tarehe 02/01/2014.
- Mapendekezo hayo yalitakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa upande wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar, mapendekezo yalitakiwa kuwasilishwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Na.
|
Kundi/Taasisi
|
Taasisi zilizoleta mapendekezo
|
Idadi ya Watu Waliopendekezwa
|
Idadi ya Wajumbe Wanaotakiwa
|
Idadi ya Walioteuliwa
|
|||
Tanzania Bara
|
Zanzibar
|
Tanzania Bara
|
Zanzibar
|
Tanzania Bara
|
Zanzibar
|
|||
1. | Taasisi zisizokuwa za Kiserikali | 246 | 98 | 1,203 | 444 | 20 | 13 | 7 |
2. | Taasisi za Kidini | 55 | 17 | 344 | 85 | 20 | 13 | 7 |
3. | Vyama vya Siasa vyenye Usajili wa Kudumu | 21 | 14 | 129 | 69 | 42 | 28 | 14 |
4. | Taasisi za Elimu | 9 | 9 | 84 | 46 | 20 | 13 | 7 |
5. | Makundi ya Walemavu | 24 | 6 | 97 | 43 | 20 | 13 | 7 |
6. | Vyama vya Wafanyakazi | 20 | 1 | 89 | 13 | 19 | 13 | 6 |
7. | Vyama Vinavyowakilisha Wafugaji | 8 | 1 | 43 | 4 | 10 | 7 | 3 |
8. | Vyama vinavyowakilisha Wavuvi | 7 | 3 | 45 | 12 | 10 | 7 | 3 |
9. | Vyama vya Wakulima | 22 | 8 | 115 | 44 | 20 | 13 | 7 |
10. | Makundi yenye Malengo Yanayofanana | 142 | 21 | 613 | 114 | 20 | 14 | 6 |
Mapendekezo Binafsi | - | - | 118 | - | ||||
Jumla | 672 | 178 | 2,880 | 874 | 201 | 134 | 67 | |
Jumla Kuu | 850 | 3,754 |
- Sheria ya Mabadiliko ya Katiba imeweka masharti ya kuzingatiwa katika uteuzi wa wajumbe 201 wa Bunge la Maalum la Katiba. Masharti hayo ni pamoja na wajumbe wasiopungua theluthi moja wanatakiwa kutoka Zanzibar na theluthi mbili kutoka Tanzania Bara. Kwa sababu hiyo, katika wajumbe 201, wajumbe 67 watatoka Zanzibar na wajumbe 134 watatoka Tanzania Bara. Aidha, mgawanyo wa wajumbe wanawake na wanaume unatakiwa uwe nusu kwa nusu. Pamoja na hayo, wajumbe hao wawakilishe sura ya wananchi wa Tanzania kwa ufuasi wa vyama vya siasa, dini, umri, na maeneo wanayotoka. Katika mazingira haya, zoezi la kupata wajumbe 201 halikuwa rahisi hata kidogo. Mwitikio wa makundi ulikuwa mkubwa sana ikilinganishwa na nafasi zilizopo.
- Kama nilivyoeleza hapo awali, mapendekezo kutoka Tanzania Bara yalikuwa 2,880 wakati nafasi za wajumbe ni 134. Kwa upande wa Zanzibar, majina yaliyopendekezwa yalikuwa 874 ikilinganishwa na idadi ya wajumbe 67 wanaotakiwa kuteuliwa. Kwa nyongeza ya maelezo kuhusu uwingi wa mapendekezo, ni kwamba ukichukua taasisi zisizo za kiserikali kwa upande wa Tanzania Bara walipendekezwa watu 1,203, wakati nafasi zilizokuwa zinatakiwa kujazwa ni 13 tu. Kwa upande Zanzibar, taasisi zisizokuwa za kiserikali zilikuwa zimependekeza majina 444 ikilinganishwa na nafasi 7 tu zilizokuwa zinatakiwa kujazwa kutokana na taasisi hizi.
10. Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania wakishirikiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpainduzi Zanzibar wamekamilisha uteuzi wa wajumbe 201. Kabla ya kutaja orodha ya wajumbe walioteuliwa, napenda kufafanua mambo yafuatayo:
(a) Uteuzi umezingatia ushiriki wa watu wa rika zote, yaani vijana, watu wazima na wazee. Kwa ajili hiyo, wajumbe vijana yaani wenye umri wa kati miaka 22-35, ni wajumbe 35. Wajumbe wenye umri wa kati, yaani miaka 36-64, ni 145; na wajumbe wazee, yaani wenye umri wa miaka 65 na kuendelea ni 21.
(b) Sheria inataka kuwepo na uwiano sawa kwa ajumbe wanawake na wanaume. Jambo hili limezingatiwa ipasavyo, na katika orodha hii wajumbe wanawake ni 100 na wanaume 101. Kwa vile, haiwezekani kuwa na nusu mtu, ndiyo maana idadi ya wajumbe wanaume ni 101.
(c) Uwakilishi wa vyama vya siasa ambao unahitaji kila chama chenye usajili wa kudumu kiwe na wajumbe wawili umezingatiwa. Kwa kuwa kuna vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu 21, jumla ya wajumbe 42 wamechaguliwa kwa maana ya kuwa wajumbe wawili wameteuliwa kutoka katika kila chama.
Baada ya maelezo hayo ya utangulizi, ifuatayo ndiyo orodha ya wajumbe 201 wa Bunge Maalum la Katiba waliobahatika kuteuliwa:
TAASISI ZISIZOKUWA ZA KISERIKALI- (WAJUMBE 20) | |
TANZANIA BARA (13) | |
1. Magdalena Rwebangira | 2. Kingunge Ngombale Mwiru |
3. Asha D. Mtwangi | 4. Maria Sarungi Tsehai |
5. Paul Kimiti | 6. Valerie N. Msoka |
7. Fortunate Moses Kabeja | 8. Sixtus Raphael Mapunda |
9. Elizabeth Maro Minde | 10. Happiness Samson Sengi |
11. Evod Herman Mmanda | 12. Godfrey Simbeye |
13. Mary Paul Daffa | |
TANZANIA ZANZIBAR (7) | |
1. Idrissa Kitwana Mustafa | 2. Siti Abbas Ali |
3. Abdalla Abass Omar | 4. Salama Aboud Talib |
5. Juma Bakari Alawi | 6. Salma Hamoud Said |
7. Adila Hilali Vuai | |
TAASISI ZA KIDINI- (WAJUMBE 20) | |
TANZANIA BARA (13) | |
1. Tamrina Manzi | 2. Olive Damian Luwena |
3. Shamim Khan | 4. Mchg. Ernest Kadiva |
5. Sheikh Hamid Masoud Jongo | 6. Askofu Mkuu (Mstaafu) Donald Leo Mtetemela |
7. Magdalena Songora | 8. Hamisi Ally Togwa |
9. Askofu Amos J. Muhagachi | 10. Easter Msambazi |
11. Mussa Yusuf Kundecha | 12. Respa Adam Miguma |
13. Prof. Costa Ricky Mahalu | |
TANZANIA ZANZIBAR (7) | |
1. Sheikh Thabit Nouman Jongo | 2. Suzana Peter Kunambi |
3. Sheikh Nassoro Mohammed Ibrahimu | 4. Fatma Mohammed Hassan |
5. Louis Majaliwa | 6. Yasmin Yusufali E. H alloo |
7. Thuwein Issa Thuwein | |
VYAMA VYOTE VYA SIASA VYENYE USAJILI WA KUDUMU – (WAJUMBE 42) |
|
TANZANIA BARA (28) | |
1. Hashim Rungwe Spunda | 2. Thomas Magnus Mgoli |
3. Rashid Hashim Mtuta | 4. Shamsa Mwangunga |
5. Yusuf S. Manyanga | 6. Christopher Mtikila |
7. Bertha Ng’angompata | 8. Suzan Marwa |
9. Dominick Abraham Lyamchai | 10. Mbwana Salum Kibanda |
11. Peter Kuga Mziray | 12. Isaac Manjoba Cheyo |
13. Dr. Emmanuel John Makaidi | 14. Prof. Ibrahim Haruna Lipumba |
15. Modesta Kizito Ponera | 16. Prof. Abdallah Safari |
17. Salumu Seleman Ally | 18. James Kabalo Mapalala |
19. Mary Oswald Mpangala | 20. Mwaka Lameck Mgimwa |
21. Nancy S. Mrikaria | 22. Nakazael Lukio Tenga |
23. Fahmi Nasoro Dovutwa | 24. Costantine Benjamini Akitanda |
25. Mary Moses Daudi | 26. Magdalena Likwina |
27. John Dustan Lifa Chipaka | 28. Rashid Mohamed Ligania Rai |
TANZANIA ZANZIBAR (14) | |
1. Ally Omar Juma | 2. Vuai Ali Vuai |
3. Mwanaidi Othman Twahir | 4. Jamila Abeid Saleh |
5. Mwanamrisho Juma Ahmed | 6. Juma Hamis Faki |
7. Tatu Mabrouk Haji | 8. Fat –Hiya Zahran Salum |
9. Hussein Juma | 10. Zeudi Mvano Abdullahi |
11. Juma Ally Khatibu | 12. Haji Ambar Khamis |
13. Khadija Abdallah Ahmed | 14. Rashid Yussuf Mchenga |
TAASISI ZA ELIMU- (WAJUMBE 20) | ||
TANZANIA BARA | ||
1. Dr. Suzan Kolimba | 2. Prof. Esther Daniel Mwaikambo | |
3. Dr. Natujwa Mvungi | 4. Prof. Romuald Haule | |
5. Dr. Domitila A.R. Bashemera | 6. Dr. Jasmine Bendantunguka Tiisekwa | |
7. Prof. Bernadeta Kilian | 8. Teddy Ladislaus Patrick | |
9. Dr. Francis Michael | 10. Prof. Remmy J. Assey | |
11. Dr. Tulia Ackson | 12. Dr. Ave Maria Emilius Semakafu | |
13. Hamza Mustafa Njozi | ||
TANZANIA ZANZIBAR (7) | ||
1. Makame Omar Makame | 2. Fatma Hamid Saleh | |
3. Dr. Aley Soud Nassor | 4. Layla Ali Salum | |
5. Dkt. Mwinyi Talib Haji | 6. Zeyana Mohamed Haji | |
7. Ali Ahmed Uki | ||
WATU WENYE ULEMAVU-(WAJUMBE 20) | ||
TANZANIA BARA (13) | ||
1. Zuhura Musa Lusonge | 2. Frederick Msigala | |
3. Amon Anastaz Mpanju | 4. Bure Zahran | |
5. Edith Aron Dosha | 6. Vincent Venance Mzena | |
7. Shida Salum Mohamed | 8. Dr. Henry Mwizengwa Nyamubi. | |
9. Elias Msiba Masamaki | 10. Faustina Jonathan Urassa | |
11. Doroth Stephano Malelela | 12. John Josephat Ndumbaro | |
13. Ernest Njama Kimaya | ||
TANZANIA ZANZIBAR (7) | ||
1. Haidar Hashim Madeweyya | 2. Alli Omar Makame | |
3. Adil Mohammed Ali | 4. Mwandawa Khamis Mohammed | |
5. Salim Abdalla Salim | 6. Salma Haji Saadat | |
7. Mwantatu Mbarak Khamis | ||
VYAMA VYA WAFANYAKAZI-(WAJUMBE 19) | ||
TANZANIA BARA (13) | ||
1. Honorata Chitanda | 2. Dr. Angelika Semike | |
3. Ezekiah Tom Oluoch | 4. Adelgunda Michael Mgaya | |
5. Dotto M. Biteko | 6. Mary Gaspar Makondo | |
7. Halfani Shabani Muhogo | 8. Yusufu Omari Singo | |
9. Joyce Mwasha | 10. Amina Mweta | |
11. Mbaraka Hussein Igangula | 12. Aina Shadrack Massawe | |
13. Lucas Charles Malunde | ||
TANZANIA ZANZIBAR (6) | ||
1. Khamis Mwinyi Mohamed | 2. Jina Hassan Silima | |
3. Makame Launi Makame | 4. Asmahany Juma Ali | |
5. Mwatoum Khamis Othman | 6. Rihi Haji Ali | |
VYAMA VINAVYOWAKILISHAWAFUGAJI-(WAJUMBE 10) | ||
TANZANIA BARA (7) | ||
1. William Tate Olenasha | 2. Makeresia Pawa | |
3. Mabagda Gesura Mwataghu | 4. Doreen Maro | |
5. Magret Nyaga | 6. Hamis Mnondwa | |
7. Ester Milimba Juma | ||
TANZANIA ZANZIBAR (3) | ||
1. Said Abdalla Bakari | 2. Mashavu Yahya | |
3. Zubeir Sufiani Mkanga | ||
VYAMA VINAVYOWAKILISHAWAVUVI –(WAJUMBE 10) | ||
TANZANIA BARA (7) | ||
1. Hawa A. Mchafu | 2. Rebecca Masato | |
3. Thomas Juma Minyaro | 4. Timtoza Bagambise | |
5. Tedy Malulu | 6. Rebecca Bugingo | |
7. Omary S. Husseni | ||
TANZANIA ZANZIBAR (3) | ||
1. Waziri Rajab | 2. Issa Ameir Suleiman | |
3. Mohamed Abdallah Ahmed | ||
VYAMA VYAWAKULIMA-(WAJUMBE 20) | ||
TANZANIA BARA (13) | ||
1. Agatha Harun Senyagwa | 2. Veronica Sophu | |
3. Shaban Suleman Muyombo | 4. Catherine Gabriel Sisuti | |
5. Hamisi Hassani Dambaya | 6. Suzy Samson Laizer | |
7. Dr. Maselle Zingura Maziku | 8. Abdallah Mashausi | |
9. Hadijah Milawo Kondo | 10. Rehema Madusa | |
11. Reuben R. Matango | 12. Happy Suma | |
13. Zainab Bakari Dihenga | ||
TANZANIA ZANZIBAR (7) | ||
1. Saleh Moh’d Saleh | 2. Biubwa Yahya Othman | |
3. Khamis Mohammed Salum | 4. Khadija Nassor Abdi | |
5. Fatma Haji Khamis | 6. Asha Makungu Othman | |
7. Asya Filfil Thani | ||
WATU WENYE MALENGO YANAYOFANANA – (WAJUMBE 20) | ||
TANZANIA BARA (14) | ||
1. Dr. Christina Mnzava | 2. Paulo Christian Makonda | |
3. Jesca Msambatavangu | 4. Julius Mtatiro | |
5. Katherin Saruni | 6. Abdallah Majura Bulembo | |
7. Hemedi Abdallah Panzi | 8. Dr. Zainab Amir Gama | |
9. Hassan Mohamed Wakasuvi | 10. Paulynus Raymond Mtendah | |
11. Almasi Athuman Maige | 12. Pamela Simon Massay | |
13. Kajubi Diocres Mukajangwa | 14. Kadari Singo | |
TANZANIA ZANZIBAR (6) | ||
1. Yussuf Omar Chunda | 2. Fatma Mussa Juma | |
3. Prof. Abdul Sheriff | 4. Amina Abdulkadir Ali | |
5. Shaka Hamdu Shaka | 6. Rehema Said Shamte | |
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
7 Februari, 2014
Jumatano, 5 Februari 2014
TAARIFA YA KUKATIKA KWA MAWASILIANO YA VODACOM
Dar es Salaam, 5 Februari, 2014.Tunapenda kuwaomba radhi wateja wetu wote kwa kushindwa kutoa huduma za mawasiliano kuanzia asubuhi ya Februari 5, 2014. Hii imetokana na kukatika kwa mkonga wa mawasiliano ulioko barabara ya Morogoro na nyingine mbili za ziada zilizoko Mlalakuwa na Mayfair plaza barabara ya Mwai kibaki jijini Dar es Salaam.
Kukatika kwa Mkonga huo kumesababisha vituo vyetu vya kutoa huduma za mawasiliano vilivyopo Oysterbay na mbezi juu kushindwa kufanya kazi kutokana na vituo hivyo kutegemeana kumesababisha kushindwa kutoa huduma za mawasiliano.
Kutokana na hilo wateja hawakuwa na uwezo wa kupiga simu, kutumia intaneti na hata huduma za kifedha. Tunatambua usumbufu ambao umetokea kwa kukosa mawasiliano, kwa mara nyingine tena tunaomba radhi na tunashukuru kwa uvumilivu wao katika kipindi chote ambacho huduma zilikosekana.
Mafundi wetu wameweza kurekebisha uharibifu uliotokea barabara ya Mwai kibaki ambao uliotokana na shughuli za ujenzi wa barabara zinazoendelea. Uharibifu mwingine uliotokea katika Barabara ya Mlalakuwa ulichukua muda kurekebisha kutokana na nyaya zilizo katika mkonga wa mawasiliano kuungua kulikosababishwa na zoezi la uchomaji taka lililokuwa linaendelea katika sehemu ambayo mkongo umepita na kusababisha uharibifu huo.
Napenda kuwahakikishia wateja wetu kuwa, Tumejidhatiti katika kuendelea kutoa huduma bora na za kipekee wakati wote watakapokuwa wanautumia mtandao wa Vodacom, Tunawashukuru kwa namna ambavyo wameendelea kutuunga mkono na kutuvumilia pale matatizo yanapojitokeza.
Rene Meza
Mkurugenzi Mtendaji – Vodacom Tanzania
Kilichosemwa na Basata kuhusu kufungiwa kwa video kadhaa hapa Bongo ikiwemo ya Snura.
Siku kadhaa zilizopita kupitia millardayo.com kuna taarifa ziliztoka kuhusu kufungiwa kwa video ya Nimevurugwa ya Snura,taaarifa hizi alizi-amplify meneja wake Snura ‘Hk’ akidai kuwa sababu maalum bado hawajazipata ingawa kila kituo anachoenda wanampa sababu tofauti.
Millardayo.com haikuishia hapo ilienda moja kwa moja kwenye Baraza la Sanaa la Taifa(Basata)ili kuujua undani wa sakata hili ikiwemo pia kuulizia video ya Jux(uzuri wako)ambayo nayo ilitoka taarifa ya kufungiwa kwa video hiyo.
Kutoka Basata huyu hapa Godfrey mungeleza ni kaimu katibu mtendaji anataarifa zaidi>>Unaposema kufungia video moja kwa moja kuna chombo kingine cha serikali kinashughulikia hilo ambao ni bodi ya filamu Tanzania’
‘Bodi ya filamu wanaangalia video zote suala zima la filamu wanapoona hii haikidhi au haifai kwa jamii za Kitanzania basi wanaisimamisha kidogo wanamshauri aweze kuirekebisha ili iweze kulingana na maadili ya kitanzania’
‘Sisi tunaangalia Audio kabla haijaingia sokoni katika urasimishaji tunakaa tunausikiliza muziki wake tunashauriana kwamba akarekebishe hapa na tunaangalia mambo mengi ikiwemo ubunifu wake mwenyewe’
‘Suala la kufungiwa kwa Snura najua kabisa linaenda kwenye suala la maadili na limeandikwa sana na sisi Baraza kama Baraza tunaangalia sana suala la maadili tukisema tunamfungia hatufungii video tu tunamfungia msanii mwenyewe’
BAADA YA BAADHI KUJIUNGA CCM-BONGO MOVIES VIPANDEVIPANDE!
Stori: Waandishi Wetu
MPASUKO mkubwa umeikumba tasnia ya filamu Bongo baada ya baadhi ya wasanii wanaong’ara kuchukua kadi rasmi za kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), Risasi Mchanganyiko linakupa zaidi.
Tukio hilo lilitokea juzi, Jumapili jijini Mbeya kulipokuwa na sherehe za maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho ambapo mgeni rasmi alikuwa ni mwenyekiti wa chama hicho taifa, Rais Jakaya Kikwete.
Mashabiki mbalimbali wa sinema za Kibongo, waliingia kwenye mjadala mkubwa katika mitandao ya kijamii, mara baada ya wasanii hao kuonesha uamuzi wao, kila mmoja akieleza mtazamo wake.
WASANII WENYEWE
Baadhi ya wasanii waliochukua kadi za CCM ni pamoja na Jacob Steven ‘JB’, Single Mtambalike ‘Richie’, Irene Uwoya, Haji Salum ‘Mboto’, Tamrina Posh ‘Amanda’, Blandina Chagula ‘Johari’, Wastara Juma na Haji Adam ‘Baba Haji’.
MIJADALA
Watoa maoni walikuwa na mawazo tofauti kuhusiana na uamuzi wa wasanii hao wenye mashabiki wengi, wengine wakiwapongeza huku upande wa pili ukiwashutumu kwa maelezo kuwa wanawagawa mashabiki wao.
Mtoa maoni aliyejitaja kwa jina la Mussa Juma aliandika: “Sijui hawa wasanii wetu watakua lini? Huwezi kuonesha itikadi yako ya kisiasa wakati una mashabiki wengi. Hapo wamechemka. Mfano mimi siyo CCM na siwezi kununua tena filamu za JB.”
IPYANA LWIGA:
“Hii ndiyo demokrasia, unawavuta watu wajiunge kwako kwa kuwapa usafiri na mahitaji yote muhimu! Wameona mbali sana, nawapongeza sana! Wajifunze kwa Marlaw!”
BENATUS MARWA NYAMBORI:
“Huo ni uamuzi wao. Hauhusiani na kazi zao. Kama umechukia, chukua kazi zao zote piga moto. Kiukweli Chadema mnafikiri watu wengi wanawasapoti? Hapana... huko vijijini wanakuja kuangalia helikopta maana hawajawahi kuiona.”
JACOBS KING:
“Sasa hivi ndiyo watakoma kabisa, najua hakuna wa kununua kazi zao, wataibiwa mpaka wakome, CCM wanataka kuwatumia kwenye kampeni mikoani ili wawavutie wananchi kwenye mikutano yao lakini kwa sasa Watanzania tunajielewa.”
COCU BATENGA:
“Wasanii wana haki ya kuchagua chama chochote wakipendacho. Wakati wa kazi ni kazi, siasa ni siasa. Mbona Sugu (Joseph Mbilinyi – Mbunge wa Mbeya Mjini) yupo bungeni? Mbona Afande Sele (Seleman Msindi) ametangaza kujiunga Chadema, mbona hayasemwi? Hakuna mantiki hapa.”
JB BUNGENI
Hivi karibuni, JB alitangaza nia yake ya kugombea ubunge ingawa bado hajataja jimbo, kitendawili cha atagombea kwa tiketi ya chama gani, kimeshateguka baada ya kuchukua kadi ya CCM.
Hata hivyo, minong’ono inasema kwamba, JB huenda atagombea Jimbo la Kinondoni (kwa sababu ndiyo eneo analoishi) au Same (kwa sababu ni mzaliwa wa huko).
TUNDU LISSU:WABUNGE WENGI BONGO HAWAJUI KINGEREZA
Mbunge wa Singida Mashariki, mnadhimu wa upinzani na mwanasheria mkuu wa CHADEMA mh. Tundu Lissu, amesema kuwa wabunge wengi wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania hawajui lugha ya kiingereza kitendo kinachowafanya wakose ufanisi katika kazi zao za kibunge hususani mijadala mbalimbali bungeni na nje ya bunge.
Mwanasheria huyo amekiita kitendo hicho kuwa ni janga la taifa ambapo ameshauri suala hilo litazamwe upya ili tuwe na wabunge wanaoweza kuwa tija kwa taifa.
Ikumbukwe kuwa wabunge wengi wa bunge hili wamekuwa wakituhumiwa kuwa na elimu za kidato cha nne (iv) au chini ya hapo na wengine kidato cha sita chenye matokeo mabaya.
source; cluods fm na star tv.
Taarifa kuhusu hukumu ya Chris Brown na kesi ya kumshambulia mtu.
Chris Brown akiambatana na girlfriend wake Karrueche Tran pamoja na wakili wake wameingia kwenye chumba cha mahakama huko L.A baada ya ushahidi wa kesi inayomkabili kupitiwa.
Kesi hiyo ilikuwa inasema kwamba Chris Brown alimshambulia mtu mmoja huko D.C na waendesha kesi hiyo walisisitiza kwamba tabia ya Chris Brown ya kufanya fujo na kushambulia watu inaendelea kukua na kutokea mara nyingi na inaongeza hatari kwa jamii.
Licha ya mambo yote kusikilizwa na jaji James Brandlin hakukubaliana na hayo mawazo ambayo yalitaka C Brown afungwe jela. Mwisho wa kesi jaji alisema ni bora Chris Brown aendelee na siku tisini za rehab for anger management kuliko kumuweka jela.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)