.

Jumatatu, 30 Desemba 2013

IMEBIMBURUKA.... KUMBE CHANZO CHA DIAMOND NA PENNY KUACHANA NI KIGOGO WA CCM NA SIO MADAME WEMA


Imebainika kuwa kuvunjika kwa uchumba baina ya  Naseeb Abdull 'Diamond' na Penieli Mwigila kumechangiwa na kigogo mmoja wa CCM ambaye amekuwa na mahusiano ya kimapenzi na Penny!  inakupa full details.
Habari za ndani kutoka vyanzo vyetu zimebainisha kuwa tangu siku nyingi kigogo huyo wa CCM (jina tunalo) amekuwa akilifaidi penzi la mwanadada Penny kwakuwa anamkono wa birika (mgumu kwenye fedha) licha ya kwamba fedha anazo.

Akitoboa siri za ndani, mnyetishaji wetu amesema kwamba mbali ya ubahili wa Diamond pia ndugu wa upande wa Penny hawakuwa wakipenda binti yao aishi na Diamond kwa kuwa hana sifa za kuishi naye hali iliyo mrahisishia kigogo huyo kula vya watu


"Amini kwamba katika kipindi chote cha mahusiano yao, Diamond hajawahi kusalimiana na mama yake Penny hata siku moja, hata kaka zake Penny hawataki kabisa kumsikia Diamond na mara kibao wamekuwa wakimsema sana Penny kuhusu Diamond" kimesema chanzo chetu

Kikaongeza "Hata kuachana kwao ni Penny ndiye aliyemuacha Diamond kwa sababu ambazo si za msingi sana kwani siku nyingi Penny alishakata tamaa ya kuishi na Diamond

"Nakumbuka kipindi baba yake Wema alipofarikil, Diamond alitaka kwenda msibani kuzika lakini alikuwa anashindwa atamuagaje Penny, hivyo akaamua amsukumizie mzigo Babu Tale ili ampigie simu na kujifanya yeye ndiye aliyemshinikiza kwenda kuzika"

"Sasa siku Diamond alipoaga kwenda Msibani, Penny 'akamtaiti' na kumuuliza anakwenda kumzika nani? Diamond akamwambia amuulize Babu Tale lakini Penny alimgomea na kumwambia wewe ndiye unayekwenda kuzika na wewe ndiye unayenihusu nitamuuliza vipi Babu Tale?


"Diamond akawa hana cha kujibu zaidi ya kuzuga kisha baadae kuondoka na kwenda Zanzibar kuzika" kilisema chanzo hicho


Hata hivyo habri zaidi zinasema kabla ya Bifu hilo halijatokea Diamondi alikuwa amesha mpatia kiasi cha fedha Penny kwa ajili kutafuta nyumba akapange ili waishi tofauti na familia jambo ambalo Diamond aligomea kipindi alipokuwa akiishi na Wema.

"Kwa hiyo Diamond alipoondoka tu kwenda Zanzibar, Penny naye akahama nyumbani kwao akawa anaishi kwenye hotel moja Sinza, wakati mwingine alikuwa akionekana hotelini hapo na wifi yake, kipindi hicho ndipo kigogo wa CCM naye akajitanua zaidi na kuanza kumuhudumia Penny kama mkewe.

"Licha ya kwamba mama na dada wa Diamond walikuwa wakimkubali sana Penny na kujaribu kumsihi kutomwacha kijana wao lakini Penny alishakuwa ameonyesha Dalili zote za kutoishio nyumbani kwa mama Naseeb"


Kipindi Fulani Diamond alijaribu kubembeleza uchumba kwa Penny hadi akauchimba ukoo wao na kugundua kuwa baba yake Penny na Bibi yake Diamond wamewahi kuishi kijiji kimoja (huko kigoma) hivyo Diamind akazusha habari kuwa wao ni Ndugu akiamini itamsaidia kuwafanya wazazi wa Penny anafaa kumuoa binti yao lakini ugunduzi huo ukageuka kuwa kashfa mpya!" kilisema chanzo hicho.

"Kimsingi huyo kigogo niliyewatajia ndiye anahudumia Penny , fanyeni utafiti mtagundua" kilimaliza chanzo hicho

Baada ya kupata taarifa hizo ilimpigia Simu Penny ili kuweka sawa taarifa hizi lakini iliita bila kupokelewa.
 

Jitihada za kumhoji kigogo huyo zinaendelea...

ETI KUNA UKWELI WOWOTE KWAMBA AGNESS MASOGANGE ANAMUIGA HUYU DADA MIKA SHAY KATIKA MAVAZI ?


TAZAMA YALIYOJIRI KWENYE UBATIZO WA MTOTO WA MBUNGE WA JIMBO LA MBEYA ,JOSEPH MBILINYI (SUGU MOTO CHINI)


Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa(CCM), akimpatia zawadi mke wa Mbunge wa Jimbo la
Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi(Chadema).

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya, Dr. Mary Mwanjelwa na Mbunge wa Jmbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi(SUGU).

Dr. Mary Mwanjelwa siku ya ubatizo wa Mtoto Shasa Joseph Mbilinyi (Sugu) Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini (Chadema) katikati, mtoto akiwa amebebwa na mama yake Mbeya Mjini.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi



Tufurahi pamoja




Sote ni ndugu.

AMINI USIAMINI...HAPA NDIPO MWANA DADA LADY JAYDEE ALIPOZALIWA KATIKA HIKI CHUMBA



YANI RIHANNA ANAMAKUSUDI SANA,.! FULL MITEGO YANI HATARI SANA:



Rihanna amekuwa akionyesha utukutu wake mara nyingi jukwaani lakini hii ilikuwa kali alikuwa akiimba huku akionyesha makalio yake na kukatika, watu wote walibaki midomo wazi huku wakishangilia kwa
uchizi aliokuwa akionyesha msanii huyo. Show hiyo ilifanyika huko France

"Nimedata na Penzi la Mke wa mtu Jamani, Nifanyeje?"......Mdau


Jamani nimeshindwa kuvumilia mapenzi nayopewa na huyu mtoto wa kichaga, ingawa ni kweli mke wa mtu mume wa huyu dada ni mtu wa kusafiri sana mikoa mbali mbali kwa biashara zake.
 
 Tatizo limekuja pale napomwambia tuachane kwa vile ni mke wa mtu hataki hata kusikia, first time nimemtokea akanambia yupo single girl ila baaada ya siku nikawa nimegundua ni mke wa mtu.
Jamani na mimi nimedata mbaya kwa kweli cause hata min kabaaang ananipa tuu hana choyo mtoto wa watu, je nifanyaje nimwache?

Msanii Geez Mabovu sasa yupo hoi kitandani...!!



Geez Mabovu mtoto wa Doll South yuko katika hali mbaya kiafya na amelazwa katika hospitali ya mkoa wa Iringa baada ya kuzidiwa ghafla wakati akisubiri kufanya show mjini humo akiwa na Jan B na Songa. Songa ameandika kwenye ukurasa wake wa facebook kuwaopa taarifa fans wa Mabovu na kuwaomba waendelee kumuombea. “ASANTENI SANA IRINGA,SIKUTEGEMEA MNAPENDA HIP HOP KIASI KILE...MLITISHA SANA. ILA KUNA HABARI MBAYA NDUGU YETU GEEZ MABOVU HALI YAKE SIO NZURI AMELAZWA,NAOMBA TUMUOMBEE ARUDI KATIKA HALI YAKE YA 
KAWAIDA. ASANTENI” 
  Geez Mabovu alazwa katika hospitali ya mkoa wa Iringa, tumuombee apone haraka
Songa ameueleza mtandao wa Bongo5 kuwa Mabovu alizidiwa ghafla kabla ya show na akapelekwa hospitali ya mkoa. Mapema jana ,Geez Mabovu aliongea na tovuti ya Times Fm na kueleza kuwa alienda nyumbani kwao Iringa ambapo alikuwa hajaenda kwa muda mrefu na kwamba alienda kusherehekea siku yake ya kuzaliwa (December 25) na familia yake. Rapper huyo aliongeza kuwa ameamua kuacha kutumia pombe kuanzia January Mosi mwakani kutokana na kutaka kufanya mabadiliko zaidi katika maisha yake. Tumuombee Geez Mabovu apate nafuu na apone haraka.